Page 160 - Fasihi_Kisw_F5
P. 160

Fasihi ya Kiswahili  kwa Shule za Sekondari





                                Zoezi la 6.2



                 1.   Jadili hoja kwamba matumizi ya TEHAMA yana athari katika kazi za
          FOR ONLINE READING ONLY
                     fasihi ya Kiswahili.

                 2.   Jadili umuhimu wa kutumia majukwaa ya kidijiti katika kusambaza kazi
                     za fasihi ya Kiswahili.

                 3.   Kwa kutumia mifano, fafanua namna uigizaji unavyoweza kuwa fursa
                     ya kukuza uchumi.

                 4.   “TEHAMA haina  mchango  wowote katika  kuchangia miktadha  ya
                     utunzi wa kazi za fasihi”. Jadili.




               Shughuli ya 6.5
              Kwa kutumia vyanzo vya mtandaoni na maktabani, jadili hatua za utunzi wa kazi
              za kifasihi.


              Hatua za utunzi wa kazi za fasihi
              Uandishi wa kazi za fasihi huongozwa na hatua mbalimbali ambazo hutegemeana
              na kukamilishana.  Mtunzi wa maigizo,  mashairi au hadithi za watoto hana
              budi kuzingatia hatua hizo ili aweze kuandika kazi yenye ubora na ushawishi.
              Uandishi wa kazi za fasihi unaweza kujumuishwa katika hatua kuu tano ambazo
              ni:  maandalizi,  uandishi/utungaji,  uboreshaji,  uhariri,  na  mapitio  ya  mwisho.
              Ufuatao ni ufafanuzi wa hatua hizi:

              (a)  Kufanya maandalizi
              Katika  hatua ya maandalizi,  mwandishi  anaweza  kujiuliza  maswali  kadhaa
              kuhusu uandishi wake. Mifano ya maswali  hayo ni: Ni jambo  gani anataka
              kuandika?  Kwa nini aandike  kuhusu jambo  hilo? Anamwandikia  nani?  Wapi
              atapata ukweli/uhakika kuhusu mambo anayotaka kuandika? Vifaa gani muhimu
              vinahitajika katika uandishi wake? Maswali haya yanadokeza mambo muhimu
              ambayo mwandishi anapaswa kuyafanya kabla ya mchakato mzima wa uandishi.
              Hivyo, katika hatua hii, mtunzi hupaswa kubuni wazo au mada ya uandishi, na
              kuanza kufanya uchunguzi kuhusu mada hiyo, na kuamua kuhusu utanzu wa





                     Kitabu cha Mwanafunzi                                           149
                        Kidato cha Tano



                                                                                            23/06/2024   17:54
     FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd   149                   23/06/2024   17:54
     FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd   149
   155   156   157   158   159   160   161   162   163   164   165