Page 157 - Fasihi_Kisw_F5
P. 157
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
fasihi husaidia kueneza utamaduni na sanaa ya jamii husika. Hivyo, kazi za fasihi
huweza kutoa fursa mbalimbali ambazo huinua pato la mtu binafsi na taifa kwa
ujumla. Ufuatao ni baadhi ya ufafanuzi wa fursa hizo:
Fursa mojawapo ya kazi ya fasihi ya Kiswahili ni mwandishi wa vitabu vya
FOR ONLINE READING ONLY
mashairi, tamthiliya, hadithi/hadithi za watoto, riwaya na kazi nyingine za
kiubunifu kujipatia kipato. Vitabu hivi huingizwa kwenye soko la vitabu ambapo
huweza kununuliwa na kusomwa na watu mbalimbali ndani na nje ya nchi, ambapo
mwandishi hujipatia kipato na kujikimu maisha yake. Vilevile kupitia fursa hii,
mwandishi anaweza kupata umaarufu kutokana na kazi yake na ambapo anaweza
kupata fursa ya kualikwa kwenye makongamano mbalimbali ya kiubunifu, jambo
ambalo huweza kumsaidia kumwongezea uzoefu. Kadhalika, kazi bora za fasihi
huweza kuingia katika ushindani wa tuzo mbalimbali za kitaifa na kimataifa.
Zinaposhinda, mwandishi hutunukiwa tuzo ambazo aghalabu huambatana na
kipato.
Fursa nyingine ya mwandishi wa kazi za kifasihi ni kuuza nakala laini za kazi
zake katika mitandao ya kijamii, hivyo kujipatia kipato. Mwandishi anaweza
kuamua kufungua jukwaa la mtandaoni kwa ajili ya kurusha kazi mbalimbali
za fasihi alizotunga. Pia, anaweza kuingia mikataba na wamiliki wa vituo vya
runinga, redio na vyombo vingine vya habari na kupeleka kazi zake kwa ajili
ya kusomwa, kutazamwa na kusikilizwa na jamii. Fursa zote hizi si kwamba
humnufaisha mwandishi kwa kipato tu bali huweza kumpa umaarufu, hivyo watu
kupenda kazi zake. Hali hii humhamasisha mwandishi kutunga kazi nyingi zaidi
ambazo zitainua uchumi binafsi na wa kitaifa.
Kazi za kifasihi zinaweza kuchapishwa katika magazeti mbalimbali ya ndani na
nje ya nchi. Mwandishi anaweza kuingia mikataba na wamiliki wa makampuni
ya magazeti kwa ajili ya kuchapisha hadithi, riwaya, mashairi na kazi nyingine za
kifasihi kwa ajili ya kusomwa na jamii. Uzuri wa kazi husika unaweza kusababisha
kuwa na wafuasi wengi wa kazi hizo, suala linalomuwezesha mwandishi
kujipatia kipato na umaarufu katika jamii. Kwa mfano, hadithi zilizoandikwa na
Eric Shigongo zilipendwa na watu wa rika mbalimbali, kiasi cha kumwongezea
kipato na kumpa umaarufu mkubwa.
Uandishi wa kifasihi unaweza pia kumwezesha mtu kuwa mtaalamu wa kuhariri
makala na vitabu vya fasihi ya Kiswahili. Uandishi huo hutoa fursa kwa mhariri
kuwa na nafasi ya kusoma na kuhariri kazi binafsi au za mwandishi mwingine.
Hii husaidia kuboresha ubunifu, ubora wa lugha, muundo, maudhui na mtiririko
mzuri wa andiko husika kabla ya kuchapwa. Hii ni fursa nzuri katika kuimarisha
146 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 146 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 146