Page 153 - Fasihi_Kisw_F5
P. 153
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Sura
ya Kubuni kazi changamani
binafsi na cha jamii kwa ujumla.READING ONLY
Sita za fasihi
Utangulizi
Kazi za fasihi ni muhimu katika jamii kwa sababu huburudisha, huelimisha,
hueneza tamaduni mbalimbali na huchochea mawazo mapya kwa wasomaji.
Katika sura hii, utajifunza juu ya miktadha inayochagiza utunzi wa kazi
changamani za fasihi, fursa zinazotokana na kazi za fasihi; na mchango wa
TEHAMA katika kutambua fursa zinazotokana na kazi za fasihi. Pia, utajifunza
hatua na kanuni za utunzi, na kutunga kazi za fasihi simulizi na fasihi andishi.
Umahiri utakaojenga katika sura hii utakuwezesha kutunga maigizo, mashairi
FOR ONLINE
na hadithi za watoto; na kuzitumia kazi hizo kama fursa ya kujipatia kipato
Namna utunzi wa kazi za fasihi zinavyochochea maendeleo
binafsi na ya taifa kwa ujumla
Shughuli ya 6.1
(a) Kwa kutumia vyanzo vya mtandaoni na maktabani, eleza miktadha
inavyochagiza utunzi wa kazi za kifasihi.
(b) Kwa kutumia vyanzo vya mtandaoni au maktabani, kusanya kazi tano (5)
za fasihi za tanzu tofauti kisha chunguza na chambua miktadha iliyoziibua.
Miktadha ya utunzi wa kazi changamani za fasihi
Kazi za kifasihi ni matini ambazo hutumia lugha, ubunifu na vionjo vya kifasihi.
Kwa hiyo, kazi hizo ni matini ambazo huwasilishwa kwa ubunifu. Kazi hizi
hutofautiana na kazi nyingine zisizo za kifasihi kutokana na mbinu za uandishi
kama vile uundaji wa wahusika na matumizi ya lugha ya kisanaa. Kazi za kifasihi
142 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 142
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 142 23/06/2024 17:54