Page 148 - Fasihi_Kisw_F5
P. 148
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
ya Awali ya Sanaa katika Ualimu, nikizamia somo
la Kiswahili.
Mwenyekiti wa Jopo: Vyema. Kwa nini umeomba nafasi hii ya kazi?
FOR ONLINE READING ONLY
Nagona: Nimeomba nafasi hii ya kazi ya kuwa msaidizi wa
ukufunzi katika chuo hiki kwa sababu nina uwezo
na ninapenda kutumia elimu na taaluma yangu
kuwasaidia wengine kupitia taasisi hii.
Mwenyekiti wa Jopo: Bi. Nagona, kuna taasisi nyingi ambazo ungeweza
kuzitumia kutimiza shabaha na mapenzi yako
hayo, kwa nini iwe taasisi hii?
Nagona: Ndugu mwenyekiti, nimependa kuwa hapa kwa
sababu mbili. Mosi, hii ni taasisi ya ndoto yangu
kwa sababu siku nyingi nimekuwa nikiota kufanya
kazi hapa. Pili, ni sababu ya kuwapo kwa hiyo
ndoto. Nimekuwa nikiifuatilia taasisi hii tangu
nikiwa katika hatua za chini za elimu; na nimekuwa
nikishuhudia jinsi taasisi hii ilivyo tegemeo la taifa
kwa kuzalisha wataalamu wa kada mbalimbali.
Hivyo, nikapata shauku ya mimi kuwa mmoja wa
wapishi wa wataalamu hao. Sababu ya tatu ndugu
Mwenyekiti ni kuwa taasisi hii imekuwa ya kwanza
kutoa tangazo la kazi tangu nihitimu. Hivyo, kama
wasemavyo wahenga kuwa, “mvua za kwanza ndo
za kupandia”, nami niliona niichangamkie mvua
hii ya kwanza kunyesha kwa muktadha wa kusaka
ajira.
Mwenyekiti wa Jopo: Karibuni wajumbe tumuulize maswali msailiwa.
Mjumbe 1: Bi. Nagona, una kipi cha kutushawishi kuwa wewe
ni bora kuliko waombaji wengine wa nafasi hii?
Nagona: Ndugu Mwenyekiti na jopo zima, ninawahakikishia
kuwa mimi ni bora kuliko wengine kwa sababu
zifuatazo: Mosi, matokeo yaliyomo katika vyeti
vyangu vya elimu na taaluma yananibainisha
Kitabu cha Mwanafunzi 137
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 137 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 137