Page 147 - Fasihi_Kisw_F5
P. 147
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
(b) Kwa kutumia misingi ya ujenzi wa hoja zenye mantiki na ushawishi,
tathimini matendo ya wahusika katika tamthiliya teule mbili.
Kuwasilisha hoja zenye mantiki na ushawishi kwa kutumia maarifa
ya kifasihi
FOR ONLINE READING ONLY
Maarifa ya kifasihi hujumuisha umilisi wa vipera mbalimbali vya fasihi simulizi
na andishi. Kazi yoyote ya fasihi huwa na mambo yanayoweza kutumiwa katika
maisha halisi. Miongoni mwa matumizi hayo ni kujengea hoja zenye mantiki
na ushawishi. Mjenzi wa hoja za kimantiki huweza kutumia vipera kama vile
methali, hadithi, na tamathali za semi ili kukazia au kunogesha hoja yake.
Jambo muhimu ni mjengahoja kuteua kipengele cha kifasihi ambacho ni sahihi
na muafaka katika muktadha wa hoja yake. Kwa ujumla, maneno, vifungu na
tungo za kifasihi huwa na mvuto na mguso wa kipekee. Kutokana na mguso
huo, zikitumiwa kwa usahihi sambamba na misingi ya kujenga hoja za kimantiki,
hurahisisha kueleweka na kushawishi hadhira. Hoja zenye mantiki na ushawishi
zinaweza kutumiwa na watu katika sehemu mbalimbali wakati wa kueleza
au kuomba kitu fulani. Sehemu ambazo hoja za kimantiki hutumika ni kama
vile kwenye usaili wa kazi au kwenye malumbano ya hoja. Maelezo yafuatayo
yanafafanua namna hoja za kimantiki na zenye ushawishi zinavyotumika katika
usaili na malumbano ya hoja.
Kutumia maarifa ya kifasihi kuwasilisha hoja zenye mantiki na ushawishi
katika usaili
Shughuli ya 5.12
(a) Soma dayalojia ifuatayo ya usaili, kisha jibu maswali yanayofuata:
Mwenyekiti wa Jopo: Jitambulishe tafadhali.
Msailiwa: Ninaitwa Nagona Dhifa Mzingile. Nina miaka 26.
Nimezaliwa na kukulia wilayani Songea, mkoani
Ruvuma. Nilianza masomo ya msingi mwaka 2005
katika Shule ya Msingi Mpangula na kuhitimu
mwaka 2011. Kisha, nikajiunga na elimu ya
sekondari katika Shule ya Sekondari Namtumbo
na kuhitimu mwaka 2015. Baada ya hapo,
nilisoma elimu ya sekondari ya juu katika Shule
ya Sekondari ya Wasichana Songea na kuhitimu
mwaka 2018. Baadaye, nilijiunga na masomo ya
juu, ambapo mwaka 2023 nilitunukiwa Shahada
136 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 136
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 136 23/06/2024 17:54