Page 142 - Fasihi_Kisw_F5
P. 142
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
(ii) Ni mbinu zipi za kifasihi zimekutatiza kupata maana katika shairi hili?
(iii) Una maoni gani kuhusu kufaa au kutofaa kwa mbinu za kifasihi
zilizotumika katika shairi hili ili kuleta maana?
(iv) Mstari unaosema ‘Mbaya wetu karudi, shetani rangi rangile’ una
FOR ONLINE READING ONLY
maana gani?
(b) Kwa kutumia diwani teule, chambua shairi moja, kisha onesha namna
mbinu za kifasihi zilivyochangia au kutatiza kupatikana kwa maana.
Mbinu za kifasihi zinavyoathiri kupatikana kwa maana katika tamthiliya
Shughuli ya 5.9
Soma matini fupi ya tamthiliya ifuatayo, kisha chambua namna mbinu za kifasihi
zinavyoathiri maana.
Moyo: [Anaitazama hali iliyowazunguka]
Nani wa kulaumiwa? Kati ya mpunga uliosababisha viroboto au
mwenye mguu anayeshindwa kutoa funza?
[Anazama kwa tafakuri nzito].
Macho: wote.
Moyo: Ikiwa wote, tupe sababu kuntu. Kwa nini?
Macho: Wote wanaonekana. Mimi ninalaumu kila anayeonekana.
Ndani joto ni kali sana, nasema na nje baridi ni kali sana sitakaa
kimya.
Akili: Hahahah! [Kicheko], wanadunga wa kwetu, wao wanauza.
Masomo yao moshi ni sumu ya kwetu moshi ni chakula, twala na
hatushibi.
Moyo: Nani alaumiwe? Someni pale “Ni hatari kwa mustakabali
wako.” Haya niambieni, nani alaumiwe? Anayetoa ujumbe ule
ndiye anayekusanya kodi kutoka palepale.
[Anaonesha kwa kidole].
Kitabu cha Mwanafunzi 131
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 131 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 131