Page 140 - Fasihi_Kisw_F5
P. 140
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Bi Tano: [Amekasirika zaidi]: Kila nilipokwenda wananiambia
wameshanunua vya kutosha. Sasa mimi ningewalazimisha?
Bi Moja: Biashara inataka bembeleza eti.
FOR ONLINE READING ONLY
Bi Nne: Eee. Unasema maneno matamu matamu. Basi hivihivi tu watu
watanunua?
Bi Tano: Basi chukueni muende mkauze wenyewe
[Anaondoka amekasirika]
Bi Moja: Huyo Bi Tano mwacheni. Kichwa chake kibovu.
Jamani saa imekwisha. Hebu tugawane hivi vitambaa kila mtu
akauze katika eneo lake.
[Wote wanagawana vitambaa]
Bi Nne: Haya maarifa mazuri. Jamani tujitahidi tukikutana wiki ijayo kila
mtu awe ameshauza vya kwake.
Nguzo Mama (Muhando, 2007: 16–17)
Maswali
(i) Ni maana zipi zinazopatikana katika sentensi isemayo “Biashara
inataka kubembeleza eti.”
(ii) Mvutano baina ya Bi Tano na wenzake unaibua maana zipi?
(iii) Mitazamo ya wahusika katika kipande hiki cha tamthiliya inaibua
maana zipi za kiujumi?
(iv) Ni mbinu gani zimetumika kupata maana kutoka katika kipande hiki
cha tamthiliya?
(v) Ni maana zipi nyingine unazoweza kuibua kutokana na kipande hiki
cha tamthiliya?
(b) Chambua maana mbalimbali zinazopatikana katika tamthiliya mbili teule.
Kitabu cha Mwanafunzi 129
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 129 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 129