Page 143 - Fasihi_Kisw_F5
P. 143
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Macho: Kweli sio wote. Mimi nimekuwa nikishuhudia wa kwetu tu
ndo hukamatwa. Wasanii wetu, wachezaji wetu na … naa …
[Anakatishwa].
Akili: Na viongozi ni wetu.
FOR ONLINE READING ONLY
Macho: Na watoto wa viongozi.
Moyo: Watoto wa viongozi?
Macho: Watoto wetu jamani wana mambo.
Moyo: Watoto wetu au wa viongozi?
Akili: Ninakariri, wetu. [Amekaza macho]
Macho: [Anatahamaki, apiga kalele].
Nyie nyie … mnafanya ajizi na mnahisi ni madogo ingawa yana
ukubwa wake.
[Kama mtu alipandwa na mchera].
Moyo: Madogo?
Akili: Kama haya ni madogo, makubwa ni yapi?
Macho: Unataka kujua makubwa, ebu geuka kuleee. Mi naona ndoa,
Ninyi mnaona pia. Geuka huku. Ndoa yenu yawa yao
[Wote wanageukageuka huku na huku kama mazuzu].
Nje-ndani (Mswahili na Njonjolo, 2016:22)
Maswali
(i) Ni mbinu zipi za kifasihi zimekuwezesha kupata maana katika matini
hii?
(ii) Ni mbinu zipi za kifasihi zimekutatiza katika kupata maana katika
matini hii?
(iii) Una maoni gani kuhusu kufaa au kutofaa kwa mbinu za kifasihi
zilizotumika katika matini hii katika kuleta maana?
132 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 132
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 132 23/06/2024 17:54