Page 141 - Fasihi_Kisw_F5
P. 141
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Mbinu za kifasihi zinavyoathiri kupatikana kwa maana katika kazi za
fasihi
Katika machakato wa usomaji, huweza kuibuka maana tofauti kwa kila msomaji.
Jambo, hili huweza kutokana na jinsi msomaji anavyofasili taswira mbalimbali
FOR ONLINE READING ONLY
zilizotumiwa. Kuwapo kwa uwezekano wa kupatikana kwa maana mbalimbali
kunatokana na mtunzi kutumia mbinu ya kifasihi ya ufumbaji. Hii inamaanisha
kuwa, kama mtunzi asingefumba, maana ingekuwa ya wazi na ya moja kwa moja.
Hivyo, kuwapo kwa maana tofauti kunatokana na mbinu za uandishi na utungaji
ambao hufasiliwa kwa njia tofauti kwenye sehemu au kazi nzima ya kifasihi.
Mbinu za kifasihi hutumika katika kazi mbalimbali za kifasihi kulingana na nini
mtunzi anapenda kuandikia. Mbinu hizo zinabainika katika shughuli ifuatayo.
Mbinu za kifasihi zinavyoathiri kupatikana kwa maana katika mashairi
Shughuli ya 5.8
(a) Soma shairi lifuatalo, kisha jibu maswali yanayofuata:
Shetani, Rangi Rangile
Aa, awali sisi twanena, sisi sisi wananchi,
Ama kiza twakiona, ni kiza hiki hakuchi,
Mbaya wetu karudi, karudi tena mbichi,
Huu ukweli nanena, kweli siyo pirikichi,
Mbaya wetu karudi, shetani rangi rangile.
Ba, bahari tunaiona, bado haina shuwari,
Mawimbi yatatizana, mkondoni menawiri,
Tufani ni nana nana, katu hatuoni heri,
Roho atuminya sana, ka jeuri na kiburi,
Mbaya wetu karudi, shetani rangi rangile.
Diwani ya Tunzo ya Ushairi ya Ebrahim Hussein (Rashid, 2016:166)
Maswali
(i) Ni mbinu zipi za kifasihi zimetumika kupata maana katika shairi hili?
130 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 130
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 130 23/06/2024 17:54