Page 137 - Fasihi_Kisw_F5
P. 137
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
hupendwa na kila mtu ndani ya familia. Sauti yake ni ulinzi tosha dhidi ya
wapangaji wanaochungulia na kudokoa mali ya binadamu.
Rangi nzuri inayovutia pamoja na macho yake mithili ya gololi ni baadhi ya
vitu vinavyompa upekee. Paka ni doli la watoto na kitulizo murua cha watoto
FOR ONLINE READING ONLY
dhidi ya adui zao. Kiumbe huyu hukunja kucha zake vizuri ili zisimdhuru mtoto
aliyembeba. Adabu hii amefundishwa na mama yake, ndio maana wahenga
wanasema samaki mkunje angali mbichi.
Paka wetu ni mwaminifu na mlinzi bora, kwake udokozi ni mwiko. Hana tabia ya
kula chakula isipokuwa amewekewa kwenye chombo maalumu. Chakula chake
ni maziwa, michuzi na mifupa ya samaki.
Weledi wa kijasusi, paka amekirimiwa. Huweza kuwapigisha kwata maadui
aliowateka. Hawa ni wale wenye mipango ya kumpora binadamu. Paka huwaona,
kisha hutembea kwa kunyata taa! Taa! Taa! Taa! Kisha kuwarukia na kuwakamata.
Paka awapo vitani, hapati ngeu kichogoni. Ni jasiri ajabu! Asikiapo mlio wa
nyoka siii! iiii! iiii! Hujipanga haraka kwa ajili ya kumdaka nyoka mithili ya
golikipa. Siku moja, tulisikia vurugu kali juu ya dari, kumbe alikuwa nyoka
aliyekuwa akipambana na paka. Paka alifanikiwa kumuua nyoka mkubwa na
kushuka naye kutoka darini.
Usalama wa mali zetu upo mikononi mwa paka. Paka ana mbinu kabambe za
kumdhibiti rafiki yake aitwaye Panya. Wakati mwingine humwimbia nyimbo
kama:
“Njoo tule nyama, njoo ×2
Nyama hiyooo!
Kimbiaaa!
Njoo tufurahi.”
Paka hutumia mbinu hizi kuwarubuni panya na hatimaye kuwakamata. Mali zetu
ambazo ni nguo, vitabu, daftari na viatu vina usalama wa kutosha kutokana na
kuwapo kwa paka.
Paka hukwea miti kwa maringo mithili ya kinyonga afukuzaye mawindo. Hapa
126 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 126 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 126