Page 132 - Fasihi_Kisw_F5
P. 132
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
(c) Chambua mbinu zilizotumika kujenga ujumi katika mashairi mawili ya
diwani teule ulizozisoma.
Mbinu zilizotumika kujenga ujumi katika majigambo
FOR ONLINE READING ONLY
Shughuli ya 5.3
(a) Tamba au soma jigambo lifuatalo, kisha jibu maswali yanayofuata.
Jabali
Mimi ni jabali
Naangamiza kama umeme unavyopasua anga
Wenye shari wote huniogopa
Mafedhuli na mahayawani hufichama wakiniona
Kila dhalimu hunigwaya na kunikimbia
Mimi ni kama jahazi linalopambana na mawimbi baharini
Gharika ikishavuma hurudi kuwa wima
Yote yenye mawaa hukimbia kutokomea
Wengi kushangaa jabali kuwayumbisha
Madhalimu wote udhalimu hukoma
Matendo mema hutenda kuisalimisha dunia
Mimi ni jabali
kamwe sitetereki kwa lolote.
Maswali
(i) Ni kwa namna gani taswira zimetumika kujenga ujumi katika jigambo
hili?
(ii) Mbinu ya taharuki imetumikaje kujenga ujumi katika jigambo hili?
(iii) Ni vifungu vipi vya maneno katika jigambo hili vinaakisi mbinu ya
uteuzi na mpangilio wa maneno?
(iv) Ni mbinu zipi nyingine zilizotumika kujenga ujumi katika jigambo
hili?
Kitabu cha Mwanafunzi 121
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 121 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 121