Page 130 - Fasihi_Kisw_F5
P. 130
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Kila mtu lugha yake, ndiye mtumishi mwema,
Lugha nyingine makeke, mviringo kuzisema,
Kila mkuu na pake, hana hadhi akihama,
FOR ONLINE READING ONLY
Kiswahili nivike, joho lako la heshima,
Titi la mama li tamu, jingine halishi hamu.
Lugha yangu ya utoto, hata leo nimekua,
Tangu ulimi mzito, sasa kusema najua,
Sawa na manukato, moyoni mwangu na pua,
Pori, bahari na mto, napita nikitumia,
Titi la mama li tamu, jingine halishi hamu.
Kiswahili kikikopa, lugha nyingine pia,
Ambazo zimenenepa, jambo hili hutumia,
Au sivyo zingetupwa, kwa kukosa manufaa,
Kiswahili kikikopa, si ila ndiyo tabia,
Titi la mama li tamu, jingine halishi hamu.
Pambo la Lugha (Robert, 1973:27-29)
Maswali
(i) Unafikiri kwa nini mwandishi amefananisha Kiswahili na titi la mama?
(ii) Ni mbinu zipi za kiujumi zilizotumika katika shairi hili?
(iii) Ni kipengele kipi cha ujumi wa kijadi kinachojitokeza katika shairi
hili?
(iv) Katika ubeti wa pili, mwandishi anakusudia nini anapotaja lugha za
Kiarabu, Kirumi na Kiingereza?
(v) Ni dhana zipi zinazodhihirisha uzuri na ubaya wa shairi hili?
Kitabu cha Mwanafunzi 119
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 119 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 119