Page 126 - Fasihi_Kisw_F5
P. 126
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
(v) Ni kwa namna gani matendo ya wahusika Vera na Avita yanasawiri
matendo yanayofanywa na watu katika jamii?
(vi) Kiimani na kimtazamo mhusika Beti anawakilisha kundi lipi la vijana
katika jamii?
FOR ONLINE READING ONLY
(vii) Una mtazamo gani wa jumla kuhusu matini hii?
(b) Jadili athari za kiimani na kimitazamo zilizomo katika tamthiliya mbili
teule, zinavyojitokeza katika jamii.
Tamrini
1. Jadili namna athari za mitazamo ya wahusika wawili katika tamthiliya
teule mbili ulizosoma zinavyojitokeza katika jamii.
2. Jadili uhusiano uliopo baina ya mitazamo iliyomo katika nyimbo mbili
za bongo fleva na matendo ya jamii.
3. Linganisha masuala ya mitazamo ya kijamii kama yanavyosawiriwa
katika tamthiliya mbili teule.
4. Jadili kauli kwamba “Nyimbo za bongo fleva hazina maadili kwa jamii”.
5. Chambua maadili na mitazamo inayojitokeza katika mashairi mawili ya
diwani teule.
6. Tumia nyimbo mbili za bongo fleva kulinganisha mitazamo iliyomo
katika nyimbo hizo na imani za jamii.
7. Huku ukilinganisha na imani za jamii, jadili maadili yanayopatikana
katika tamthiliya mbili teule.
8. Maadili na imani za jamii zinachangia katika utunzi wa kazi za fasihi
hususani nyimbo na tamthiliya. Jadili kauli hii kwa kutumia mashairi
mawili (2) kutoka katika diwani teule.
9. Sikiliza nyimbo mbili za bongo fleva uzipendazo, kisha chambua
maadili yaliyomo katika nyimbo hizo.
10. Athari za kiimani na kimtazamo huweza kuimarisha au kudumaza kazi
za kifasihi. Jadili kauli hii kwa mifano kuntu.
Kitabu cha Mwanafunzi 115
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 115 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 115