Page 123 - Fasihi_Kisw_F5
P. 123
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Athari za kiimani na kimtazamo katika bongo fleva zinavyojidhihirisha
katika jamii
Kuna athari nyingi za kiimani na za kimtazamo zinazotokana na maudhui ya
nyimbo za bongo fleva. Kwa kuwa utanzu huu hutumia zaidi redio, runinga
FOR ONLINE READING ONLY
na mitandao ya kijamii, inakuwa rahisi kwa athari za imani na mitazamo hiyo
kuifikia hadhira kwa haraka. Athari hizo huweza kujenga ama kubomoa jamii
zisipopokelewa kwa tahadhari na uchambuzi faafu.
Shughuli ya 4.15
(a) Kwa kutumia vyanzo vya mkondoni na vinginevyo, sikiliza wimbo wa
msanii yeyote wa kike unaohamasisha mapambano ya maisha, kisha jibu
maswali yafuatayo:
(i) Ni mitazamo na imani ipi inapatikana katika wimbo huo?
(ii) Wimbo huo unatoa taswira gani kuhusiana na changamoto za kiuchumi
na maisha ya kila siku katika jamii?
(iii) Wimbo huo una athari zipi za kiimani na kimtazamo katika jamii?
(iv) Wimbo huo una athari zipi za kiimani na kimtazamo kwa vijana?
(v) Ni mitazamo ipi iliyomo katika wimbo huo haiendani na jamii? Kwa
nini?
(vi) Ni mafunzo gani jamii inaweza kuyapata kutokana na wimbo huo?
(vii) Una mtazamo gani kuhusu wimbo huo ukilinganisha na maisha ya kila
siku?
(b) Jadili namna athari za kiimani na mitazamo katika nyimbo mbili za bongo
fleva (kongwe na za sasa) zinavyojitokeza katika jamii.
Athari za kiimani na kimtazamo katika mashairi zinavyojitokeza katika
jamii
Fasihi andishi, ukiwamo utanzu wa ushairi, husawiri imani na mitazamo ya
jamii katika kutoa maudhui. Maudhui hayo huchagiza ufanisi na mabadiliko
yanayohitajika. Kwa njia hii, mashairi huibua mitazamo na imani ambazo huweza
kuchangia ustawi wa jamii husika.
112 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 112
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 112 23/06/2024 17:54