Page 122 - Fasihi_Kisw_F5
P. 122
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Che Munndu: Wasomeshe basi hao watoto wako. Nani anataka hasara?
Unapeleka watoto shule siku mbili wamepata mimba.
Bi Somoe: Lakini si nyie wenyewe ndo mwawapa mimba? We
mwenyewe mbona mwaka juzi ulioa binti ndogo wa shule.
FOR ONLINE READING ONLY
Lakini sharia zipo, iko siku zitachukua nkondo wake.
Che Munndu: Sheria sheria ndo kitu gani? Wangapi hapa kijijini
wamewapa watoto wa shule mimba. Na hatuoni kufungwa?
Si mnawafundisha watoto wenu wenyewe (huku akibana
pua) ‘bwana aliyenipa mimba sinjui’. Sasa hiyo akili
kweli? Hela yangu si afadhali nkaoe nke mwingine.
Kuliko kupeleka ntoto shule anayeishia kupata mimba na
kuniongezea nzigo?
Safari ya Chinga (Omari, 2012: 18 – 20)
Maswali
(i) Mwandishi anabainisha mitazamo gani katika kipande hiki cha
tamthiliya?
(ii) Una maoni gani kuhusu mitazamo iliyomo katika kipande hiki cha
tamthiliya? (Toa sababu)
(iii) Unafikiri mtazamo wa mhusika Bi. Somoe una uhalisi katika jamii?
Kwa nini?
(iv) Je, unadhani mtazamo wa Che Mundu wa kujitenga na jukumu la
kumuelimisha mtoto unasawiri matendo ya jamii yako?
(v) Ni kwa namna gani mitazamo ya mhusika Che Mundu inaathiri
matendo ya jamii?
(vi) Je, jamii yako ina mitazamo gani kuhusu mimba za utotoni?
(vii) Unafikiri kuna uhusiano wowote kati ya mitazamo ya wahusika wa
tamthiliya hii na matendo ya jamii? Toa sababu.
(b) Kwa kutumia tamthiliya mbili teule ulizosoma, husianisha mitazamo
iliyomo katika tamthiliya hizo na matendo ya jamii.
Kitabu cha Mwanafunzi 111
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 111 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 111