Page 127 - Fasihi_Kisw_F5
P. 127
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Sura
ya Ujumi katika kazi za fasihi
FOR ONLINE READING ONLY
Tano
Utangulizi
Ujumi ni dhana inayotumika duniani kote japo wananadharia na wanajamii
hutofautiana kimtazamo kuhusu dhana hii. Mijadala kuhusu ujumi hujitokeza
katika nyanja tofauti, miongoni mwa nyanja hizo ni fasihi andishi na simulizi.
Katika sura hii, utajifunza kueleza na kuchambua mbinu za kiujumi katika
kazi za fasihi za majigambo, mashairi na tamthiliya teule. Aidha, utajifunza
jinsi mbinu za kifasihi zinavyoathiri kupatikana kwa maana katika kazi hizo.
Kadhalika, utajifunza namna ya kutumia fasihi katika kujenga hoja zenye
mantiki na ushawishi. Umahiri utaoujenga utakuwezesha kutambua na kueleza
ujumi katika miktadha mbalimbali.
Namna uchambuzi wa ujumi unavyoboresha utunzi wa kazi
za fasihi
Shughuli ya 5.1
Kusanya nyimbo tano (5) za bongo fleva ambazo, kwa maoni yako, ni nzuri na
nyimbo tano (5) ambazo, kwa maoni yako, ni mbaya; kisha, kwa kila wimbo
eleza kwa nini unaona ni mzuri au mbaya.
Ujenzi wa ujumi katika kazi za fasihi
Dhana ya ujumi imejadiliwa na wataalamu mbalimbali kwa mfano Zirimu na
Gurr (1971), Nyirenda na Ishumi (2002), Ponera (2014), na Habwe na Zaja (2019)
ambao wanaeleza kuwa ujumi ni hisia za akilini au ni misingi ya kifalsafa kuhusu
uzuri wa sanaa. Wanaongeza kuwa ujumi sharti uendane na jamii mahsusi kwa
lengo mahsusi la kazi ya kisanaa inayobuniwa. Nyirenda na Ishumi (2002) wote
116 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 116
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 116 23/06/2024 17:54