Page 131 - Fasihi_Kisw_F5
P. 131
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
(b) Chambua mbinu zilizotumika kujenga ujumi katika shairi lifuatalo.
Ukurasa wa Mwisho
Nimesoma visa vya mazonge ya vituko, mazinge ya njia;
FOR ONLINE READING ONLY
Visa vya ndoto zenye matundu, macho mia yanayougua;
Visa vya pesa kuzidi kujaa kwenye mifuko is’ojaa;
Na ukata kustakimu ubavuni pa ukwasi dawamu;
Nimevisoma na kusaili;
Ukurasa wa mwisho haupo?
Nimesoma visa vya wakata misitu ya majoka yatishayo;
Visa vya mazimwi yalayo watu, na vifisi na vibweha vyayo;
Visa vya kina Masalakulangwa - adui wa mazimwi hayo;
Visa vya wajenzi nyumba mpya, na walimaji mashamba mapya;
Nimevisoma na kung’amua:
Ukurasa wa mwisho haupo.
Nimesoma ngano isiyokuwa na mwisho - ya maendeleo
Ya mnyonge katika mazonge ya mawimbi ya bahari leo;
Ngano ngumu ya sanaa ya harakati iwashayo mifuo
Ya jasho na nyundo na risasi, - tabaka kuasi kwa visasi
Nimesoma, na sasa nakiri:
Ukurasa wa mwisho haupo.
Nimezisoma pia ngano za kale zisizosahaulika
Za matamanio yasiyokauka, na ari is’ovunjika;
Nimesoma jinsi ya kufumbua ishara zilizofumbika;
Nazidi kufunua kurasa, nazidi kufasiri mikasa:
Nimesoma, na sasa nasema:
Ukurasa wa mwisho haupo.
Kunga za Ushairi na Diwani Yetu (Kahigi na Mulokozi, 1979:118-119)
120 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 120 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 120