Page 135 - Fasihi_Kisw_F5
P. 135
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
(iv) Ni vifungu vipi vya maneno katika tamthiliya hii vinaakisi mbinu ya
uteuzi na mpangilio wa maneno?
(v) Ni mbinu zipi nyingine za kiujumi zimetumika katika matini hii?
FOR ONLINE READING ONLY
(b) Chambua mbinu zilizotumika kujenga ujumi katika tamthiliya teule mbili
ulizosoma.
Maana na matumizi ya lugha katika matini za fasihi
Kazi yoyote ya fasihi huwa na maana. Mtunzi hukusudia kuwasilisha ujumbe
fulani kwa hadhira anayoilenga. Matini ya kifasihi hutofautiana na matini isiyo
ya kifasihi (kama vile taarifa ya habari iwasilishwayo katika chombo cha habari)
kutokana na matumizi ya lugha ya kifasihi. Lugha hiyo ya kifasihi hupatikana
kutokana na matumizi ya mbinu za kifasihi. Baadhi ya mbinu hizo ni: semi (kama
vile methali na nahau), tamathali za semi (kama vile sitiari, majazi, tashibiha, na
tashihisi), mafumbo, lugha ya ishara na alama, na uteuzi na mpangilio maalumu
wa maneno. Kutokana na matumizi ya mbinu hizi, matini ya kifasihi huwa na sifa
ya kufikirisha kuliko matini isiyo ya kifasihi. Pia, mbinu hizo huifanya kazi ya
fasihi iwe na mvuto kwa hadhira yake.
Hali ya hadhira kuwa na uwezo tofauti pamoja na kuwapo kwa lugha ya kifasihi
katika matini husababisha hadhira kuibua maana tofauti katika matini moja.
Hivyo, ili hadhira ipate maana iliyokusudiwa, hutakiwa kuwa na uwezo wa
kung’amua maana mbalimbali ambazo zimefumbatwa katika mbinu hizo. Maana
huweza kujitokeza katika kazi za kifasihi kama vile insha za kifasihi, mashairi na
tamthiliya kama ifuatavyo:
Maana zinazopatikana katika insha za kifasihi
Shughuli ya 5.5
(a) Soma insha ifuatayo, kisha jibu maswali yanayofuata.
Uongo
Uongo ni kinyume cha hakika ya mambo yaliyokuwa au yalivyo. Ni
watu wachache ambao si waongo katika dunia. Watakaokudanganya au
kukupunja hutumia uongo. Huweza kumsaidia mtu kujiokoa pengine, lakini
ni mamoja yote kuwa uongo ni tabia mbaya na si kitu cha kupendelea katika
maisha. Uongo hautazamiwi kwa watu waovu na wajinga peke yao, hata
watu wema na wataalamu huutumia. Bahari moja ya hatari katika dunia ni
uongo. Mwongo mmoja huweza kuangamiza watu kadha wa kadha. Uongo
wa wajinga hugunduliwa upesi sana kuliko ule wa wataalamu. Baadhi ya
124 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 124
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 124 23/06/2024 17:54