Page 134 - Fasihi_Kisw_F5
P. 134
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Wakati unaojibadilisha kama kinyonga,
Wakati unaofuata mahitaji ya wavunja-sheria
Na wafuata-sheria wakati mmoja, sawia;
FOR ONLINE READING ONLY
Kufuata mahitaji na himaya ya nafsi moja dhidi ya
nyingine …
Wakati unaowaridhi wawamba-ngoma …
Wakati wenye moyo wa kusubiri mpaka nukta ya mwisho
ifike …
Hata ikiwa miaka, karne kwa karne …
Kungojea mwisho wa mwanzo, utakaposema:
“Ho! Sasa basi tena … hatesi mtesi na kufululiza …”
Wakati, mhodhi wa matatizo
Na unaoona leo na kesho
Na hatimaye kulipa baina ya wagomvi wawili
Baina ya nguvu mbili zinazovutana …
Bi. Kirembwe: Hakika wakati si wangu tena … (Anapiga kelele na kulia
huku akijibanza kipembeni …)
Kivuli Kinaishi (Mohamed, 1990:128-129)
Maswali
(i) Ni kwa namna gani mbinu ya utanzia imetumika kujenga ujumi katika
matini hii?
(ii) Mbinu ya taharuki imetumikaje kujenga ujumi katika matini hii?
(iii) Ni kwa namna gani mbinu ya ujadi imetumika kujenga ujumi katika
matini hii?
Kitabu cha Mwanafunzi 123
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 123 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 123