Page 133 - Fasihi_Kisw_F5
P. 133
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
(b) Kwa kutumia maktaba au kifaa chochote cha kidijiti, pakua kazi yoyote
ya majigambo, kisha chambua mbinu ambazo mtunzi amezitumia kujenga
ujumi katika kazi hiyo.
Mbinu zilizotumika kujenga ujumi katika tamthiliya
FOR ONLINE READING ONLY
Shughuli ya 5.4
(a) Soma matini ifuatayo, kisha jibu maswali yanayofuata.
Miguu ya Bi. Kirembwe: Na mimi pia nilichukuwa kwenye miendo yako ya
kichawi ya kuhusudu na kuangamiza…
Bi. Kirembwe: Na miguu pia? (Anaishika miguu) Nisaidieni! (Anaiendea
hadhira, lakini zile sauti za nje zinajongea karibu)
Sauti Nyingi: (Kutoka nje ambako zinajongea ndani) Sisi ni vizazi vipya
vya Gininigi,
Vizazi vya walioangamia …
Vizazi vya waliodidimia …
Sisi sasa tuna kinywa kipana …
Tuna uwezo wa kuamua tunavyotaka,
Kuamua wenyewe … kwa maslahi ya sote …
Hatutachagizwa tena na uchawi,
Tunakuja … tunakuja …
Bi. Kirembwe: Jamani wazuieni … (Anaiambia hadhira), jamani wazuieni
wasije kuni …
(Anatetemeka)
Sauti: Ah, hata wewe Bi. Kirembwe leo unagwaya?
Unatetemeka kama unjukuti unaopeperushwa na upepo?
Unalia kama mtoto mchanga au mwanamke aliyefiwa na
mumewe? Unahofu matokeo ya matendo yako mwenyewe
…
Huu, kama ulivyokwisha sema, ni mchezo wa wakati:
122 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 122
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 122 23/06/2024 17:54