Page 129 - Fasihi_Kisw_F5
P. 129
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
masimulizi, mavazi, vyakula, maudhui ya Kiafrika, pamoja na mienendo
mbalimbali ya Kiafrika.
Uchambuzi wa mbinu zilizotumika kujenga ujumi katika kazi za fasihi
FOR ONLINE READING ONLY
Mbinu zinazotumika katika kujenga ujumi huweza kuchambuliwa katika kazi
za kifasihi kama vile mashairi, tamthiliya na majigambo. Mbinu hizi za kifasihi
huipa kazi husika ujumi ambao humfanya msomaji au mtazamaji kuvutiwa
au kutokuvutiwa nao. Mbinu hizo hujitokeza katika kazi za kifasihi kama
inavyodhihirika katika shughuli zifuatazo:
Mbinu zilizotumika kujenga ujumi katika mashairi
Shughuli ya 5.2
(a) Soma shairi lifuatalo, kisha jibu maswali yanayofuata:
Kiswahili
Titi la mama li tamu, hata likiwa la mbwa,
Kiswahili naazimu, sifayo inayofumbwa,
Kwa wasiokufahamu, niimbe ilivyo kubwa,
Toka kama chemchemu, furika palipozibwa,
Titi la mama li tamu, jingine halishi hamu.
Lugha kama Kiarabu, Kirumi na Kiingereza,
Kwa wingi zimeratibu, mambo ya kupendeza,
Na mimi nimejaribu, kila hali kujifunza,
Lakini sawa na bubu, nikizisema nabezwa,
Titi la mama li tamu, jingine halishi hamu.
118 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 118 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 118