Page 128 - Fasihi_Kisw_F5
P. 128
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
wanakubaliana kwamba ujumi ni utambuzi wa uzuri au ubaya katika maumbile
asilia, vitu aundavyo mtu na sanaa. Tajiriba za kiujumi zinazoibuliwa katika akili
au hisia za mtu hujumuisha kuajabia au kufurahisha au kupendezewa au kuvutiwa
kwa uzuri wake. Kipimo cha uzuri wa kitu hujengeka katika utambuzi (kiakili na
FOR ONLINE READING ONLY
kihisia) wa mtu katika makuzi au malezi yake. Kipimo hiki hakihusu uzuri tu bali
pia ubaya wa kitu; na ubaya huu hujumuisha upungufu katika umbile au sanaa.
Kama ilivyo kwa jambo au kitu chochote, kazi ya fasihi pia huweza kuonwa
kama nzuri au mbaya. Watunzi huhakikisha kuwa kazi zao zinakuwa na thamani
ya kiujumi, yaani hadhi na mvuto kwa hadhira. Watunzi hao huujenga ujumi
kwa kutumia mbinu mbalimbali za kibunifu. Mifano ya mbinu hizo ni: taharuki,
ufutuhi, utanzia, utomeleaji, ujenzi wa wahusika, usawiri wa mandhari pamoja
na uteuzi na mpangilio mzuri wa maneno. Matumizi ya mbinu hizi huifanya kazi
ivutie na iwe na upekee. Mbinu nyingine ya kujenga ujumi katika kazi ya fasihi
ni kuzingatia vipengele vya kijadi. Watunzi hutumia ujadi katika vipengele kama
vile majina au mandhari yanayojulikana na hadhira. Ujadi vilevile hutokana na
uzoefu na tajriba ya hadhira. Mathalani, uzuri wa hadithi au ngano zenye mhusika
sungura unatokana na kukidhiwa kwa matarajio ya hadhira kwamba lazima
mhusika huyu atafanya ujanja fulani. Ikiwa mhusika huyu atatumika vinginevyo,
hadhira inaweza isiuone uzuri wa hadithi au ngano uliozoeleka kijadi kuhusu
ujanja wa sungura. Kufanya hivi kunaifanya hadhira ijione iko karibu sana na
kazi. Mbinu nyingine ni kuzingatia uhalisi. Mtunzi anapotunga kazi inayoakisi
mambo ya kweli yanayotokea katika jamii ya hadhira yake huifanya kazi iwe na
thamani kwa hadhira hiyo. Zaidi, kazi hutakiwa kuzingatia maadili ya hadhira
inayolengwa. Kazi inayoheshimu miiko au inayoepuka mambo yanayokatazwa
na jamii huwa na thamani zaidi kwa hadhira kuliko inayokiuka maadili.
Mbinu nyingine inayoweza kutumika ni ile ya mtazamo wa Kiafrika kuhusu
ujumi. Katika kulishughulikia suala la ujumi wa Kiafrika, Wafula na Njogu
(2007) wamebainisha misingi kadhaa ya ujumi huo. Baadhi ya misingi hiyo ni:
(i) Fasihi ya Kiafrika isifu Uafrika na kutilia mkazo utamaduni wa Kiafrika na
usawa wa watu wote.
(ii) Mashujaa wa Kiafrika na ushujaa wao vioneshwe katika kazi za kisanaa na
fasihi ya Kiafrika kwa jumla.
(iii) Lugha za Kiafrika zitumike katika uandishi wa fasihi ya Kiafrika.
(iv) Mbinu za utunzi zifungamane na mazingira ya Kiafrika. Mbinu hizo
zihusishe matumizi ya vitu kama vile matumizi ya mibuyu, mikuyu,
Kitabu cha Mwanafunzi 117
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 117 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 117