Page 124 - Fasihi_Kisw_F5
P. 124
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Shughuli ya 4.16
(a) Kwa kutumia vyanzo vya mkondoni au vinginevyo, sikiliza wimbo wowote
wa bongo fleva kisha jibu maswali yafuatayo:
FOR ONLINE READING ONLY
(i) Chambua dhamira za wimbo huo.
(ii) Je, ni athari zipi za kiimani na kimtazamo zinazopatikana katika
wimbo huo?
(iii) Ni mitazamo gani inasawiriwa katika wimbo huo na ina athari zipi
katika jamii?
(iv) Ni mitazamo ipi katika wimbo huo inasawiri au haisawiri jamii yako?
(v) Una mtazamo upi wa jumla kuhusu wimbo huo?
(b) Chambua athari za kiimani na kimitazamo zilizomo katika mashairi mawili
ya diwani teule, kisha thibitisha namna zinavyojitokeza katika jamii.
Athari za kiimani na kimtazamo katika tamthiliya zinavyojitokeza kwenye
jamii
Maudhui ya tamthiliya huwa na athari za kiimani na za kimtazamo ambazo
hujitokeza kwenye jamii husika. Maudhui hayo husambaa kupitia runinga, redio,
na mitandao ya kijamii. Njia hizi zinarahisisha kusambaa kwa athari hizo na
kuifikia hadhira kwa haraka.
Shughuli ya 4.17
(a) Soma matini fupi ya tamthiliya ifuatayo, kisha jibu maswali yanayofuata.
Avita: Nina wengine, siyo mwingine. Kwa uzuri huu wanaonitaka ni
wengi, lazima nibadili ladha.
Vera: Hayo ndiyo maneno, unanipa raha best. Hahahaaaa!
Avita: Tena siku hizi nina yule aliyekuwa wako ukamwacha ulipokwenda
chuo. Vipi na wewe huko chuoni umeshaopoa madaktari wangapi?
Vera: Siyo madaktari tu, na maprofesa.
Avita: Maprofesa? Sikuwezi. Unawapataje na madigrii yao vichwani?
Vera: Uzuri best, uzuri, chema chajiuza.
Kitabu cha Mwanafunzi 113
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 113 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 113