Page 119 - Fasihi_Kisw_F5
P. 119
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
(i) Unapata mitazamo gani unaposikiliza wimbo huo?
(ii) Ni matendo gani katika jamii yanaakisi mtazamo alionao mtunzi wa
wimbo huo?
(iii) Je, mitazamo ya wimbo huo inaathiri vipi jamii yako?
FOR ONLINE READING ONLY
(iv) Ni mitazamo gani katika wimbo huo unafikiri haisawiri matendo
yaliyomo katika jamii?
(v) Kuna funzo lolote unalipata kutokana na mitazamo inayoibuliwa na
mtunzi wa wimbo huo? Kwa nini?
(b) Tumia vifaa vya TEHAMA, sikiliza nyimbo za bongo fleva zisizopungua
mbili (2), kisha husianisha mitazamo iliyomo kwenye nyimbo hizo na
matendo ya jamii.
Uhusiano wa mitazamo iliyomo katika mashairi na matendo ya jamii
Mashairi mengi husawiri matendo ya jamii ambayo kwayo mafunzo na maadili
hujitokeza. Watunzi wengi wanaposana kazi zao hulenga jamii ibadilike
kimatendo ili kuleta mabadiliko, mafanikio na ufanisi unaohitajika. Endapo jamii
itazingatia matendo mazuri na kuondokana na hali ya mazoea mabaya, itachangia
katika ustawi wa mtu binafsi na jamii kwa jumla.
Shughuli ya 4.13
(a) Soma shairi lifuatalo, kisha jibu maswali yanayofuata.
Edita usinihini, naomba kusema haya
Yanishangaza machoni, kuyaficha jambo baya
Hadi naona huzuni, amefanya kwa kinaya
Mtesi mtu mbaya, hatari kuwa kundini
Hatari kuwa kundini, mtesi mtu mbaya
Muongo hawezekani, sifa yake ni ubaya
Hata akiwa jirani, kamata huu wasiya
Mtesi mtu mbaya, hatari kuwa kundini
108 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 108
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 108 23/06/2024 17:54