Page 114 - Fasihi_Kisw_F5
P. 114
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
inayojitokeza katika nyimbo za bongo fleva husambaa haraka katika jamii kupitia
majukwaa mbalimbali, yakiwamo yale ya mitandao ya kijamii. Ijapokuwa mingi
ya mitazamo hiyo ni chanya, bado kuna baadhi ya nyimbo zenye mitazamo hasi
inayosababisha zifungiwe na mamlaka husika.
FOR ONLINE READING ONLY
Shughuli ya 4.9
(a) Kwa kutumia vyanzo vya mtandaoni na vinginevyo, sikiliza wimbo wa
bongo fleva wa msanii yeyote unaosawiri athari za starehe, kisha jibu
maswali yafuatayo:
Maswali
(i) Wimbo huo una dhamira zipi?
(ii) Mtunzi ana mtazamo gani kuhusu starehe?
(iii) Jamii yako ina mitazamo gani kuhusiana na starehe zinazofanywa
katika jamii?
(iv) Mitazamo ya mtunzi wa wimbo huo inahusianaje na ile ya jamii yako?
Fafanua
(v) Una mtazamo gani kuhusu wimbo huo?
(b) Kwa kutumia vyanzo vya mtandaoni au vinginevyo, sikiliza nyimbo mbili
za bongo fleva, kisha chambua mitazamo inayopatikana katika nyimbo hizo.
Mitazamo iliyomo katika mashairi
Watunzi wa mashairi ya Kiswahili wameibua mitazamo mbalimbali kupitia kazi
zao. Baadhi ya mitazamo hiyo inasawiri maisha halisi, na inawataka wanajamii
kubadilika ili kuwa na jamii yenye ustawi na uwajibikaji. Kupitia utanzu huu,
wanajamii hujifunza kuhusiana na mitazamo iliyomo katika jamii.
Shughuli ya 4.10
(a) Ghani au soma shairi lifuatalo, kisha chambua mitazamo iliyomo.
Natamka Tanzania
Nimejaliwa mabonde natamka Tanzania,
Kama Rufiji upande, wa Mashariki sikia,
Mazao mengi ja kunde, kumbe mngejilimia,
Lakini Watanzania, bado masikini mno.
Kitabu cha Mwanafunzi 103
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 103 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 103