Page 113 - Fasihi_Kisw_F5
P. 113
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Mtendaji kata: Ondoka! Unaniwekea kiwingu, nina kazi nyingi za
kufanya.
Megno: Nimekuja kuchukua fomu, nataka kugombea
FOR ONLINE READING ONLY
Mtendaji kata: Wala usijisumbue kunieleza, ondoka. Wewe ni kilema.
Utamwongoza nani?
Megno: Tafadhali mzee sikuja kudhalilishwa utu wangu.
Mtendaji kata: Nimesema hakuna fomu. (Akisema kwa ukali) Ondoka
nisikuone!
Megno: Nashukuru sana mzee. (Megno anaondoka wakati mtendaji
anaendelea kupekua mafaili yake).
Changamoto (Mahenge, 2010: 5 - 6)
Maswali
(i) Mhusika Mtendaji ana imani gani kuhusu Megno?
(ii) Ni kwa namna gani maadili ya tamthiliya hii yanahusiana na imani za
jamii?
(iii) Jamii inaamini nini kuhusu tukio la kumfukuza Megno?
(iv) Una mtazamo gani juu ya mhusika Megno ukizingatia suala la imani
za jamii yako?
(v) Mhusika Megno anaamini nini kuhusu hali yake?
(b) Chambua uhusiano uliopo kati ya maadili na imani katika tamthiliya mbili
teule.
Mitazamo iliyomo katika bongo fleva, mashairi na tamthiliya
Watunzi wa kazi za kifasihi husawiri mitazamo mbalimbali waliyonayo au
iliyomo katika jamii. Hivyo, utunzi wa kazi zao huzingatia mitazamo hiyo na
hukusudia kuishirikisha jamii. Mitazamo hiyo imeweza kujidhihirisha katika
baadhi ya kazi za kifasihi kama vile nyimbo za bongo fleva, mashairi na
tamthiliya.
Mitazamo iliyomo katika bongo fleva
Bongo fleva ni utanzu pendwa zaidi kwa watoto, vijalunga na watu wazima. Huu
ni miongoni mwa tanzu zinazosambaa kwa haraka zaidi ikilinganishwa na tanzu
nyingine za fasihi simulizi. Kutokana na hali hii, ni wazi kwamba mitazamo
102 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 102
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 102 23/06/2024 17:54