Page 108 - Fasihi_Kisw_F5
P. 108
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Ngahinyana: (Huku akicheka): Ehe ... Ehee ... Wazee wakati mwingine
huwa tuna hasira. Kuna barua yetu? Kutoka Dalisalaam?
Pata: Nadhani inatoka Dar es Salaam. (Anapekuapekua barua
FOR ONLINE READING ONLY
hatimaye anaipata). Hii hapa. Haya mzee nakwenda.
Ngahinyana: Asante sana. Pole sana kwa kukupiga; nisamehe
mwanangu.
Pata: Si kitu mzee. (Anatoka) Siku nyingine usinivizie nyuma ya
mlango. Ningoje tuonane macho kwa macho. (Anatoka)
Mama Huka: (Anacheka): Hee ... he ... he ... Ooiii! Unaona sasa,
nilikuambia mimi. Umempiga mtoto wa watu bure.
Atapita kusema kila mahali.
Ngahinyana: Basi na wewe ... (Anachana barua na kuisoma.)
Mama Huka: Inatoka kwa shemeji?
Ngahinyana: Ee! Anashtuka na kutoa macho). Mh!
Mama Huka: Nini (Anamsogelea.)
Ngahinyana: Mh, (Huku akitikisa kichwa). Sikiliza. (Anasoma.) Kwa
kaka mpenzi,
Natum... ma... ininy... temu wa... zi... makusu...dihasa...
la...ku...waa... ndi... kiani... kuwa... aa... ri...fuma.. mbo..
fu.. lani... kuhu.. Huka. (Anaendelea kusoma hivyo
akikwamakwama). Kwanza hakuchaguliwa kuendelea na
shule. Pia, Huka, nasikitika, kuwaeleza, kuwa amebomoa
nyumba ya watu. Nina maana amewagombanisha Bi.
na Bwana Kambanga hata wameachana. (Anaachia
hapo. Anamwelekea Mama Huka). Unaona jinsi
mwanao anavyofanya. Tulikuwa tukisema sasa hivi.
(Anageuka kumwita Huka). Unaona, alipofika yule
Kitabu cha Mwanafunzi 97
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 97 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 97