Page 107 - Fasihi_Kisw_F5
P. 107
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Shughuli ya 4.4
(a) Soma matini fupi ya tamthiliya ifuatayo, kisha jibu maswali yanayofuata.
Huka: (anaanza kulia.)
FOR ONLINE READING ONLY
Ngahinyana: Eeh! Ukweli unauma sasa...
Mama Huka: Aaa, Baba Huka, usimfikirie mtoto mambo mabaya.
Ngahinyana: Hapana. Huyu mtoto amekwishaanza kuharibika. Mara
nyingi, nimeandikiwa barua na babake mdogo kusema
Huka hatulii, na wewe hukuamini ukasema wanaanza
kumsingizia mtoto wako, mpaka tukagombana na
aliyekuwa akitusomea barua zetu. (Mara hodi inasikika).
Ehee! Sasa utaniona; nitamnyosha barabara. (Anachukua
fimbo yake iliyokuwa ikiegemea ukutani na anakwenda
karibu na mlango na anainua fimbo kungojea ishuke mara
tu apigaye hodi atakapoingia.) Karibu. Fungua mlango.
Mama Huka: Hapana baba Huka! (Anamshika lakini anasukumwa). Si
vizuri.
Ngahinyana: Sogea huko! (Mgeni anaingia na fimbo ya mzee inashuka
na kutua begani mwake). Wewe ndiye ...
Pata: (Anaanguka kwa uchungu na barua alizozishika
zinatapakaa chini.) Ochchchch! Mzee vipi? Nimekukosea
nini? Ahaa (Anainuka na kushika bega lake. Ndipo
Ngahinyana anapogundua kosa lake. Huka baada ya
kuona barua anatoka).
Ngahinyana: Oh! Pole sana mwanangu, sikujua kama ni wewe.
Tulikuwa tunamtegemea mpumbavu mmoja. Lakini
bahati yake. Pole sana mwanangu! (Anasaidia kuokota
barua).
Pata: Loo! Pameuma. Pole tu haisaidii kitu. Mzee siku nyingine
uwe na uhakika au la tutaogopa kukuletea barua zako.
Unaonesha kuwa ni mkali sana!
96 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 96 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 96