Page 103 - Fasihi_Kisw_F5
P. 103
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
maamuzi, tabia na uhusiano wa watu katika maisha ya kila siku. Baadhi ya
watunzi na waandishi wa kazi za sanaa huyapa kipaumbele maadili katika
kazi zao. Kutokuzingatia misingi ya maadili katika utunzi wa kazi za kifasihi
huchangia kumomonyoka kwa maadili katika jamii. Hivyo basi, misingi hiyo
FOR ONLINE READING ONLY
inapaswa kuzingatiwa katika utunzi wa kazi mbalimbali za kifasihi, zikiwamo
nyimbo za bongo fleva mashairi na tamthiliya.
Misingi ya maadili katika jamii
Misingi ya maadili huweza kutofautiana baina ya jamii moja na nyingine. Hata
hivyo, kuna misingi ya jumla ambayo hutawala katika jamii mbalimbali. Baadhi
ya mifano ya misingi hiyo ni heshima, utii, haki na usawa, uwajibikaji, uaminifu
na uwazi:
(i) Heshima: ni hali ya kujithamini na kuwathamini wengine, mali na
mazingira yao. Heshima huweza kujengwa kwa ukarimu, uvumilivu,
uelewa na kuthaminiana miongoni mwa watu. Aidha, heshima
hudumisha umoja, amani, maelewano, nidhamu na maendeleo ya
jamii.
(ii) Utii: kipengele cha maadili ambacho huhusiana na nidhamu na
kukubali maagizo au majukumu ambayo mtu hupewa, aghalabu na
mtu aliye juu yake kiumri au kimamlaka. Pia, utii huendana na kuafiki
au kutekeleza sheria au miongozo ya kijamii. Msingi huu wa uadilifu
huleta maendeleo katika jamii na huchochea kuwapo kwa umoja na
ushirikiano.
(iii) Haki na usawa: katika jamii yenye haki na usawa, watu wanapaswa
kuwa salama, wenye uhuru kamili, na wasio na hofu ya kudhulumiwa
wala kutengwa. Haki na usawa hulinda watu dhidi ya ubaguzi wowote,
kwa misingi ya rangi, jinsi, dini, au utaifa. Kila mmoja ana thamani
na mchango katika kuleta maendeleo ya jamii yake. Hivyo, jamii
inayotambua haki na usawa hutoa elimu bora, huduma za afya na fursa
za kiuchumi kwa usawa ili kujenga maisha bora kwa mtu mmojammoja
na wanaomzunguka.
(iv) Uwajibikaji: unahusu kutimiza majukumu kikamilifu na kwa wakati.
Kila mtu anapaswa kutekeleza majukumu yake ili kuleta tija na
maendeleo katika jamii.
92 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 92
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 92 23/06/2024 17:54