Page 101 - Fasihi_Kisw_F5
P. 101
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
3. Kwa kutumia mifano ya kutosha, tofautisha mitazamo ya kidhanifu na
kiyakinifu kuhusu fani na maudhui.
4. “Nadharia za kifasihi humlemaza mhakiki”. Jadili.
FOR ONLINE READING ONLY
5. “Usomaji na uelewa wa kazi fulani ya fasihi hutofautiana baina ya mtu
mmoja na mwingine”. Thibitisha kauli hii kwa kuchambua tamthiliya
teule moja huku ukitumia nadharia ya mwitiko wa msomaji.
6. Chagua nadharia mbili za kihakiki kisha uzitumie kuchambua tamthiliya
mbili teule.
7. “Suala la ukandamizaji na unyanyasaji wa wanawake katika jamii
linapigiwa kelele na waandishi mbalimbali wa kazi za fasihi”. Tumia
nadharia ya ufeministi kuthibitisha kauli hiyo kwa kuhakiki tamthiliya
teule mbili.
8. Hakiki tamthiliya teule mbili za waandishi chipukizi kwa kutumia
nadharia ya mwingilianomatini.
9. “Hakuna jamii isiyokuwa na matabaka”. Tumia nadharia ya umaksi
kuhakiki kauli hiyo katika tamthiliya teule mbili.
10. “Kwa kuwa kila msanii na msomaji wa kazi za fasihi ni mhakiki, hakuna
haja ya kuwa na mtu anayejiita mhakiki”. Kubali au kanusha dai hili kwa
hoja maridhawa.
90 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 90
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 90 23/06/2024 17:54