Page 96 - Fasihi_Kisw_F5
P. 96
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Basi baba yako katuachia kichwa cha tembo. Tumewinda
pamoja. Jamaa zake amewapa meno na usinga. Na sisi
ametuachia kichwa cha tembo. Sasa naelewa kwa nini hakutia
saini hati. Mwenyekiti sasa hivi anatayarisha mazishi ya
FOR ONLINE READING ONLY
Herbert.
Anataka kumzika Herbert Kikiristo. Hiyo ni dhima yetu. Ni
dhima yangu. Anataka kumzika Herbert na kuandikisha kila
kitu katika jina la Umma Klan.
Kila kitu. Nyumba, viwanja, gari, fanicha kila kitu.
Unavyotuona hapa, sisi ni maskini. Ndiyo maisha ya
mwanamke. Unapoteza mume. Unapoteza maisha. Unapoteza
kila kitu.
(Kimya)
Na wewe unafanya nini? Unalialia tu hapa. Utaniona mimi
kulia? Unaniona mimi kujiuliza maswali ya kijinga? Hapana!
Kwa sababu najuwa mimi nani? Na wajibu wangu ni nini?
(Kimya)
Kweli, kuna wakati hata mimi natamani ningekuwa maiti,
simo katika maisha, nikaepukana na ujinga huu.
(Anabadilisha sauti. Anakumbuka)
Ingekuwa uzuri ningekufa siku ile nilipokuwa msituni. Ilikuwa
siku za Mau Mau. Nilikuwa naumwa malaria kali sana. Scouts
walikuwa wanatutafuta. Walipata habari wapi tumejificha.
Wenzangu wote walikimbia. Wapiganaji wawili, Njiru na
mwenziwe, walipigwa risasi wakafa palepale msituni. Mimi
nikajikokota. Nikajificha kwenye kichaka, kwenye majani.
Scouts wakaja mpaka pale nilipokuwa. Ajabu! Sikuogopa.
Nilikuwa tayari mimi kufa.
(Kimya)
Ingekuwa uzuri ningekufa! Ningekufa peke yangu kuliko hivi.
Watu chungu nzima! Rafiki tele! Bure tu. Jamaa zangu damu
moja. Wamenitenga siku ya ndoa.
Kitabu cha Mwanafunzi 85
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 85 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 85