Page 99 - Fasihi_Kisw_F5
P. 99
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Kutokana na kufanya shughuli ulizopewa, na kujibu maswali uliyoulizwa, utakuwa
umejifunza namna ya kuzitumia nadharia za umaksi na mwingilianomatini katika
kuhakiki kazi za fasihi.
Shughuli ya 3.17
FOR ONLINE READING ONLY
Kwa kutumia kazi za ushairi au tamthiliya teule, eleza mchango wa nadharia ya
mwingilianomatini katika maendeleo na uhakiki wa tanzu hizo.
Kutathmini mchango wa nadharia teule za uhakiki wa kazi za fasihi
katika maendeleo ya ushairi na tamthiliya
Kila utanzu wa fasihi hupitia mabadiliko yanayotokana na sababu mbalimbali.
Sababu hizo huweza kuwa za kijamii, kisiasa, kiutamaduni, kiuchumi, na
kitaaluma. Yote haya huathiri pia maendeleo na kukua kwa taaluma ya uhakiki
ambapo wahakiki huwa na wigo mpana wa kuibua na kutumia nadharia
mbalimbali za kihakiki. Mathalani, katika utanzu wa ushairi mabadiliko
yaliyotokea hadi kuibua mvutano baina ya washairi wa kijadi/kimapokeo na
wa kisasa ulichangia katika kuibua mawazo na aina mpya ya ushairi. Kutokana
na hali hii maana ya ushairi wa Kiswahili ilibadilika. Halikadhalika, utanzu
wa tamthiliya ulipitia mabadiliko yaliyotokana na udadisi na ubunifu wa
wanatamthiliya na wahakiki waliosaili utunzi unaofuata kanuni za Kiaristotle.
Utanzu wa tamthiliya za Kiswahili ukaanza kutumia kanuni za kijadi za fasihi
simulizi, sanaa za maonesho za Kiafrika, pamoja na kuakisi mazingira ya
Kiafrika. Mchakato huo uliibua tamthiliya za Kiswahili zenye ladha ya Kiafrika.
Mabadiliko na maendeleo ya tanzu za ushairi na tamthiliya yaliathiri na kuibua
nadharia mbalimbali za uhakiki zilizochangia maendeleo ya tanzu hizi. Nadharia
hizi zimeendelea kutumika kama mwongozo wa jumla katika kujenga hoja
wakati wa kuhakiki kazi mbalimbali za fasihi. Vilevile, nadharia hizi humsaidia
mhakiki kuibua na kuchochea udadisi katika kubaini changamoto mbalimbali
zinazoikabili jamii. Halikadhalika, nadharia humsaidia mhakiki kuchunguza
na kuifahamu jamii katika nyanja mbalimbali, kama vile za kiuchumi, kisiasa,
kiutamaduni na kijamii. Aidha, nadharia humsaidia mhakiki kujenga hoja na
kumwezesha kuweka bayana changamoto au matatizo yanayoikumba jamii. Pia,
humwezesha mhakiki kugundua au kuboresha jambo jipya. Kwa msingi huo,
nadharia ni muhimu sana katika maendeleo ya kazi mbalimbali za fasihi.
88 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 88
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 88 23/06/2024 17:54