Page 95 - Fasihi_Kisw_F5
P. 95
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Chris: Ma! Mimi nani?
Martha: Wewe? (Kimya) Wewe Chris.
Chris: Chris! Chris! (Ana uchungu) Haunielewi. Na maana:
FOR ONLINE READING ONLY
Mimi hasa ni nani? Bado haujaelewa.
Martha: Naelewa. Unatoka kusikiliza maneno ya wahuni
barabarani.
(Baada ya muda)
Mimi Martha. Wewe Chris.
Chris: Kila ukiniandikia barua, ukizungumza kwenye simu,
unanieleza habari ya familia. Iko wapi familia? Mbona…
Martha: Sitaki maneno hayo.
(Kimya)
Chris: (Anasikitika)
Baba, maskini, baba!
Martha: Mwisho… Jambo la mwisho kabisa baba yako angependa
kusikia… ni huku kuomboleza, kuomboleza.
Chris: Baba yangu? Kwani kweli baba yangu?
(Kibao)
Martha: Sijui huko Amerika wanafundisha nini? Ukitoka nje,
ukirudi mara hili. Sasa hujui mimi nani, wewe nani?
Umechanganyikiwa. Unalialia na kupenga makamasi tu hapa.
Lakini utakua kweli wewe, ukawa mtu hasa wa kukutegemea?
Baba zima. Litazame. Utaweza kushika madaraka ya aina
yoyote wewe? Utaweza kusimama mahali pa baba yako?
Chris: Kushika mahali pa baba? Nani atanisikiliza? Nitaanzaje?
Huku siko… siko kokote!
(Analia)
Martha: Msikilize, hana hata haya. Unajua maana ya kuachiwa kichwa
cha tembo? Haujui.
84 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 84
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 84 23/06/2024 17:54