Page 94 - Fasihi_Kisw_F5
P. 94
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Mume
Aaa! nimetambua, tumtafute Uledi,
Ili apike chakula, afue nguo nyumbani,
FOR ONLINE READING ONLY
Akitandike kitanda, adeki na sebule,
Haya maisha ya ndoa, wenzangu mnaishije?
Nguo zetu kunyoosha, anifunge yangu tai,
Viatu vyako kuvaa, afunge yangu lesani,
Mke wangu pumzika, kwa uchovu wa kazini
Haya maisha ya ndoa, wenzangu mnaishije?
Kurunzi (Mbijima, 2019: 17 – 20)
(i) Shairi hili lina nafasi gani katika kuleta usawa wa kijinsia katika jamii?
(ii) Mshororo usemao “mke msomi ni shida, wanaume tuna kazi” unaibua
hisia gani?
(iii) Ni kwa namna gani shairi hili linaipambanua hali ya mwanamke
kiuyakinifu?
(iv) Jadili uumbaji wa wahusika katika shairi hilo?
(v) Ni kwa namna gani shairi hili linaakisi maisha halisi ya jamii?
(c) Hakiki mashairi mawili kutoka katika diwani teule kwa kutumia nadharia
ya ufeministi.
Kutokana na kufanya shughuli ulizopewa, na kujibu maswali uliyoulizwa,
utakuwa umejifunza namna ya kuzitumia nadharia za umuundo na ufeministi
katika kuhakiki kazi za fasihi.
Shughuli ya 3.16
(a) Hakiki kipande cha tamthiliya kifuatacho kwa kutumia nadharia ya umaksi
ukiongozwa na maswali yanayofuata.
(Mahali ni palepale kama kwenye onesho la kwanza. Mapambo
yameondolewa. Martha amekaa kwenye kiti cha marehemu. Chris ameweka
kichwa chake katika mikono yake. Martha anajishughulisha kuandaa
chakula cha mchana)
Kitabu cha Mwanafunzi 83
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 83 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 83