Page 90 - Fasihi_Kisw_F5
P. 90
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
(b) Tazama maigizo katika runinga au vifaa vingine vya TEHAMA, kisha
chambua maigizo matatu kwa kutumia nadharia ya mwitiko wa msomaji,
huku ukiongozwa na maswali yafuatayo:
(i) Ni maana zipi zinaweza kupatikana katika maigizo hayo?
FOR ONLINE READING ONLY
(ii) Kwa maoni yako, ni miktadha gani imetumika katika utunzi wa
maigizo hayo?
(iii) Je, msomaji anaweza kupata athari zipi kutokana na maigizo hayo?
(iv) Maigizo hayo yana uhusiano gani na mazingira yako?
(v) Una maoni gani kuhusu usahihi wa maigizo hayo?
Kutokana na kufanya shughuli ulizopewa, na kujibu maswali uliyoulizwa,
utakuwa umejifunza namna ya kuzitumia nadharia za uhalisia na mwitiko wa
msomaji katika kuhakiki kazi za fasihi.
Kuhakiki mashairi kwa kutumia nadharia za kifasihi
Shughuli ya 3.14
Soma na hakiki shairi lifuatalo kwa kutumia nadharia ya umuundo.
Hutaniacha Morogoro
1. Ninapotazama saa, ni saa saba mchana,
Watu wengi wamekaa, stendi wasukumana,
Nasikia “Daa! Daa! Basi lenu mwaliona!”
Kondakta kwa kupaaa, sauti hiyo anena,
Ndipo ninapoutwaa, mfuko naingizana,
John ananiambia, “hutan’acha Morogoro!”
2. Niingiapo basini, kuna mtu anikuna,
Anipapasa begani, kama vile twajuana,
Najifanya simuoni, pilika zimenibana,
Ghafula aja usoni, namwona ana kwa ana,
Kumbe ni kijana John, ni mwanangu wa ujana,
John ananiambia, “hutan’acha Morogoro!”
Kitabu cha Mwanafunzi 79
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 79 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 79