Page 88 - Fasihi_Kisw_F5
P. 88
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
kazi ya sanaa ili kubainisha maadili, ujumbe, msimamo na falsafa ya kazi hiyo
kwa wanajamii. Kwa mujibu wa mtazamo huu, mhakiki ni mwalimu wa jamii
kwa kuwa humfundisha msomaji kuhusu yale yaliyomo katika kazi ya fasihi.
Aidha, mhakiki humweleza mwandishi kuhusu mambo yaliyomo katika kazi
FOR ONLINE READING ONLY
yake ambayo yanakubalika au hayakubaliki kwa jamii (Senkoro, 1973).
Mtazamo wa pili haumchukulii mhakiki kama mtu muhimu katika fasihi. Hii ni
kwa sababu, mwandishi ndiye mhakiki mwenyewe. Hivyo, huweza kujikosoa na
kurekebisha kazi yake mpaka anaporidhika nayo. Mtazamo huu pia huona kuwa
mhakiki anajipachika vyeo ambavyo hastahili kwa kusema kuwa ni mwalimu
wa msanii na msomaji kwa sababu wasomaji wa kazi za fasihi wana uwezo
wa kusoma na kuelewa; na hawahitaji watu wa kuwafafanulia. Kila msomaji
anaaminika kuwa na uwezo wa kuchambua kazi inayohusika; uchambuzi
hutofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Kwa mantiki hiyo, haitakiwi
kumtegemea mhakiki ambaye naye ana mawazo yake kulingana na uwezo wake
wa kuchambua na kufafanua kazi inayohusika (Mbele, 1993).
Kwa mtazamo wa kwanza, mhakiki wa kazi za fasihi ana dhima zifuatazo:
(i) Kuchambua kila kipengele cha fani na maudhui.
(ii) Kubainisha dhamira zinazotolewa katika kazi za fasihi.
(iii) Kuhimiza na kushirikisha fikra za kihakiki kwa wanataaluma wengine.
(iv) Kukuza kiwango cha usomaji wa kazi za fasihi.
(v) Kumwelekeza msomaji ili apate maarifa zaidi.
(vi) Kufafanua nadharia zilizotumika katika kuhakiki kazi husika.
(vii) Kubainisha misingi bora ya uandishi wa kazi za fasihi.
(viii) Kuonesha uzuri na upungufu wa kazi iliyohakikiwa kwa lengo la kuelimisha
jamii na waandishi wa kazi za fasihi.
Zoezi la 3.2
1. Eleza tofauti kati ya nadharia na nadharia za uhakiki wa kazi za fasihi.
2. Jadili kwa kutumia mifano umuhimu wa nadharia za uhakiki wa kazi za
fasihi.
Kitabu cha Mwanafunzi 77
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 77 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 77