Page 86 - Fasihi_Kisw_F5
P. 86
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Shughuli ya 3.11
Kwa kutumia vyanzo vya mtandaoni na maktabani, fafanua maana na misingi ya
nadharia ya mwingilianomatini katika kuhakiki kazi za fasihi.
Nadharia ya mwingilianomatini
FOR ONLINE READING ONLY
Nadharia ya mwingilianomatini inahusu namna matini moja inavyohusiana na
matini nyingine. Kwa jumla, nadharia hii husisitiza kwamba kila kazi ya kifasihi
kwa namna moja au nyingine inahusiana na kazi iliyoandikwa kabla au kazi
nyingine mbalimbali. Katika uhusiano huo, vipengele vya kifani na kimaudhui
vya kazi moja ya mwanzo huathiri kazi mpya kwa namna ambayo huonesha
kufanana kwa vipengele vya kazi hizo.
Nadharia ya mwingilianomatini iliasisiwa na Julia Kristeva (1941 hadi sasa)
kutokana na mawazo aliyoyapata katika nadharia ya usemezano iliyoasisiwa na
Mikhail Bakhtin (1895-1975). Kristeva anaitazama dhana ya mwingilianomatini
kama jumla ya maarifa na mbinu zinazoifanya maana ya matini moja kueleweka
kwa kuhusisha na matini nyingine.
Misingi ya nadharia ya mwingilianomatini
Ifuatayo ni misingi ya nadharia ya mwingilianomatini:
(i) hakuna matini inayoweza kuchunguzwa peke yake kwa kujitegemea, bali
lazima pawe na matini nyingine iliyotangulia inayohusiana na matini hiyo
mpya;
(ii) matini za kifasihi huchota, hunukuu, hugeuza, na kuiga kwa namna ya
kubeza au kurejelea kwa njia moja au nyingine; na
(iii) kazi za kifasihi huundwa kutokana na tamaduni mbalimbali zinazopatikana
katika matini mbalimbali za kifasihi na zisizo za kifasihi.
Kwa hiyo, unapohakiki kazi ya fasihi kwa kutumia nadharia ya mwingilianomatini
unatakiwa kuangalia uhusiano wa matini moja na matini nyingine kwa kutumia
ulinganishi wa vipengele vya kifani na kimaudhui katika kazi mpya na zile za
awali. Kwa mfano, unaweza kuchunguza namna wahusika walivyochorwa, jinsi
mandhari yanavyoathiri tabia na matukio katika kazi ya fasihi, matukio mbalimbali
ya kihistoria, mtindo na mbinu za uandishi, mwingiliano wa kiutamaduni, na
uwasilishwaji wa maudhui. Pia, unaweza kuchunguza mwingiliano wa fasihi
simulizi na andishi, mwingiliano wa tanzu, na mwingiliano wa vipera.
Kitabu cha Mwanafunzi 75
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 75 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 75