Page 82 - Fasihi_Kisw_F5
P. 82
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
(iii) watunzi wa kazi za fasihi kuwa na jukumu la kufichua, kudadisi na
kukosoa mifumo ya kibwanyenye;
(iv) kuwapo kwa kupigania haki za mtu/jamii; na
(v) kubainisha vipengele kama vile maadili, itikadi, dini na utamaduni na
FOR ONLINE READING ONLY
namna vinavyoathiri maisha ya jamii.
Unapochambua kazi ya kifasihi kwa kutumia nadharia ya umaksi, unatakiwa
kuchunguza namna mwandishi anavyoibua harakati za kitabaka katika kazi hiyo,
mifumo ya uzalishaji mali, namna kazi hiyo inavyodadisi mambo mbalimbali
katika jamii, na kupigania haki za mtu/jamii. Pia, unatakiwa kuhakiki vipengele
mbalimbali vya maisha (maadili, itikadi, dini na utamaduni), migongano ya
kijamii, na muundo wa jamii kwa kuangalia hali ya uchumi wao. Zaidi, unatakiwa
kubainisha msimamo wa mwandishi wa kazi hiyo katika kuleta mabadiliko kwa
jamii. Iwapo unachambua tamthiliya kama vile Kwenye Ukingo wa Thim (Hussein
1988), Nguzo Mama (Muhando 1982), Kivuli Kinaishi (Mohamed 1990), na
Ngoma ya Ng’wanamalundi (Mbogo 1988), zingatia namna vipengele kama vile
migogoro ya kitabaka inavyosawiriwa hadi kupatikana kwa haki ya wanyonge.
Shughuli ya 3.8
Kwa kutumia vyanzo vya mtandaoni na maktabani, fafanua maana na misingi ya
nadharia ya ufeministi katika kuhakiki kazi za fasihi.
Nadharia ya ufeministi
Ufeministi ni nadharia iliyojikita kwenye harakati za kupigania ukombozi wa
mwanamke dhidi ya mifumo kandamizi ya kisiasa, kijamii na kiuchumi. Mifumo
hii imelenga kumkandamiza, kumnyonya na kumbagua mwanamke. Lengo la
nadharia ya ufeministi ni kubainisha vipengele vya mifumo hii ili kupata suluhu
ya matatizo yanayomkabili mwanamke katika hali mbalimbali.
Baadhi ya waasisi wa nadharia hii ni Mary Wollstonecraft (1759 - 1797), Virginia
Woolf (1882 - 1941) na Simeon de Beauvoir (1908 - 1986). Awali ufeminisiti
uliibuka kama vuguvugu la kisiasa, ambapo lengo lake lilikuwa kuwainua
wanawake kutoka katika hali ya kukandamizwa, kunyanyaswa, na kutengwa;
na hivyo, kuwawezesha kupata haki ya kujieleza. Wanafeministi wa mwanzo
walizungumzia matatizo yao kwa njia ya maandishi au machapisho na wakati
mwingine mihadhara. Walikosoa na kuzipiga vita asasi kama vile za dini, ndoa
na utamaduni zinazomdhalilisha au kumdunisha mwanamke.
Kitabu cha Mwanafunzi 71
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 71 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 71