Page 78 - Fasihi_Kisw_F5
P. 78
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
(a) Kuwavutia wasomaji
Kazi iliyopambwa kwa sanaa huwavutia wasomaji kutamani kuisoma na
kuielewa. Wasomaji hupenda kazi za fasihi ambazo huwafanya wasichoke
kusoma na wauishi ulimwengu wa kazi hiyo. Kwa mfano, kutumia mbinu nzuri
FOR ONLINE READING ONLY
za kisanaa huwezesha kufikisha ujumbe husika, kuielewa na kuifurahia kazi ya
fasihi.
(b) Kuchochea mawazo na hisia kwa wasomaji
Uandishi wenye mifano ya kina na uumbaji wa wahusika na mandhari kiubunifu
huwafanya wasomaji kuhisi na kufikiri zaidi. Kazi za fasihi zinazochochea
mawazo na kuibua hisia husaidia kuleta mabadiliko ya kifikra, kuongeza ubunifu
na maarifa, na kuwapa wasomaji mtazamo tofauti kuhusu maisha na duniani
wanamoishi.
(c) Kuipa maana kazi ya fasihi
Wasomaji wengi hupenda kufuatilia hadithi au tukio fulani na hutamani kulijua
zaidi, yamkini kutokana na mafunzo ama ujumbe uliomo ndani yake. Maudhui
yaliyomo ndani ya kazi ya fasihi huwafanya wasomaji kuutazama ulimwengu
kwa jicho la tofauti na kuwafikirisha kuhusu masuala muhimu katika jamii.
Hivyo, maudhui husaidia kubaini mafunzo yatokanayo na kazi za fasihi.
(d) Kuongeza ubora na upekee wa kazi ya fasihi
Mwandishi anayetumia ubunifu mkubwa uliojaa mbinu za kifasihi katika
mtindo wake wa uandishi huongeza ubora wa kazi na kutofautisha kazi hiyo na
nyingine. Matumizi ya tamathali za semi na taswira mbalimbali husaidia kuumba
ulimwengu mbadala ambao unaakisi ukweli na uongo, hali ambayo huzidisha
ubunifu wa kazi za fasihi.
(e) Kukuza stadi za uandishi wa kazi za fasihi
Ufahamu wa kina wa vipengele vya fani na maudhui huwasaidia waandishi
kuandika kwa umahiri mkubwa.
Zoezi la 3.1
1. “Fani na maudhui havina umuhimu katika kazi za fasihi”. Jadili hoja hii
kwa mifano thabiti kutoka katika kazi teule za fasihi.
2. Fafanua kauli kwamba “uhusiano wa fani na maudhuii ni kama chai na
kikombe”.
Kitabu cha Mwanafunzi 67
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 67 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 67