Page 75 - Fasihi_Kisw_F5
P. 75
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Sura
ya Kutathmini kazi za fasihi
FOR ONLINE READING ONLY
Tatu
Utangulizi
Kutathmini kazi za fasihi ni muhimu kwa sababu kunajenga uwezo wa kiakili na
kihisia, kukuza stadi za uchambuzi na uandishi, kuchochea mawazo na kuelewa
muktadha wa kihistoria na kijamii. Katika sura hii utajifunza, mitazamo,
uhusiano na dhima ya vipengele vya fani na maudhui katika kazi za fasihi. Pia,
utajifunza nadharia za uhakiki wa kazi za fasihi pamoja na kuzitumia katika
kuchambua kazi mbalimbali za kifasihi. Umahiri utakaoujenga katika sura hii
utakuwezesha kukuza stadi za uchambuzi na uandishi wa kazi za kifasihi.
Fani bila maudhui
Shughuli ya 3.1
Kwa kutumia vyanzo vya mtandaoni au maktabani na vinginevyo, soma matini
zinazohusu mitazamo mbalimbali ya dhana za fani na maudhui.
Mitazamo kuhusu fani na maudhui
Kuna mitazamo miwili inayoeleza fani na maudhui nayo ni: mtazamo wa
kidhanifu na wa kiyakinifu. Sehemu inayofuata inafafanua mitazamo hiyo.
Mtazamo wa Kidhanifu
Mtazamo wa kidhanifu ni ule unaochukulia fani na maudhui kama vipengele
ambavyo havina uhusiano, yaani kila kimoja kinajitegemea. Kwa mtazamo huu,
katika kazi za fasihi, fani na maudhui huweza kutenganishwa na kila kimoja
kikajitegemea. Hivyo, mtunzi anaweza kufikisha ujumbe wake kwa hadhira
aliyokusudia bila kutilia maanani fani. Sengo na Kiango (1973) na Nkwera (1978)
wametumia mtazamo wa kidhanifu katika kufasili dhana za fani na maudhui.
64 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 64
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 64 23/06/2024 17:54