Page 72 - Fasihi_Kisw_F5
P. 72
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
(b) Kuburudisha jamii
Mchango mwingine wa fasihi simulizi na andishi ni kuburudisha jamii. Katika
kutimiza jukumu hili, fasihi hustarehesha, huliwaza na kutuliza mwili na akili ya
hadhira. Kwa mfano, watu wanapotazama vichekesho na maigizo ya “Mizengwe”
FOR ONLINE READING ONLY
(katika ITV Tanzania) hufurahia vituko, kejeli na mizaha inayoigizwa.
(c) Kuutambulisha na kuendeleza utamaduni
Fasihi simulizi na andishi husaidia kuutambulisha, kuutangaza na kuuendeleza
utamaduni. Kwa mfano, kazi mbalimbali za fasihi simulizi na fasihi andishi ya
Kiswahili huakisi vipengele mbalimbali vya utamaduni wa Mswahili. Mifano ya
vipengele hivyo ni desturi, dini, mavazi, mila, vyakula, na namna ya kuhusiana.
Vilevile, mchango mwingine ni kuchangia katika kutunza amali na kumbukumbu
nyingine za jamii. Mifano ya amali hizo za kijamii ni mila, desturi, historia na
sanaa. Tamthiliya za Kiswahili kama vile Kinjekitile (Hussein, 1969) na Ngoma
ya Ng’wanamalundi (Mbogo, 1988) zimebeba vyema jukumu hili la kuhifadhi
na kurithisha amali za jamii. Pia, zinafafanua masuala ya kijadi kama vile imani
na uganga.
(d) Kuadibu na kunasihi jamii
Mara nyingi, fasihi hutumika kama nyenzo ya kuasa na kuadibu kuhusu mambo
mbalimbali yanayojitokeza katika jamii. Kwa mfano, tamthiliya ya Ngoswe Penzi
Kitovu cha Uzembe (Semzaba, 1988) inawaadibu na kuwaasa watu kufanya kazi
kwa nidhamu. Kwa ufupi, tamthiliya hiyo inatoa funzo kwamba mtaka yote
kwa pupa, hukosa yote. Katika fasihi simulizi, nyimbo hutumika kukamilisha
jukumu hili. Kwa mfano, baadhi ya nyimbo za bongo fleva zina wasihi watu
kupambana na harakati za maisha kwa kutafuta fursa za kiuchumi, bila kujali
umbali unaoweza kusababisha utengano wa kifamilia.
(e) Kukuza na kuhifadhi lugha
Fasihi simulizi na andishi ina mchango mkubwa katika kuikuza lugha. Lugha
haiwezi kudumaa kwa sababu inakuwa kwenye matumizi. Mwanafasihi hutumia
maneno kuibua na kueleza dhana mbalimbali katika utunzi wa kazi zake. Uandishi
na usimulizi wa kazi za fasihi huibua misemo mipya mara kwa mara; kwa njia hii
lugha huweza kukua. Kwa mfano, katika riwaya ya Kusadikika (Robert, 1991)
kuna uibuaji wa msamiati kama vile ‘ali ali’ (tukufu) ‘azali’ (asili au kiini) ‘kitali’
(mapigano) na ‘mlizamu’ (chemchem).
(f) Kutia hamasa jamii
Fasihi hutia hamasa kuhusiana na mambo mbalimbali yanayotendeka katika
jamii. Mathalani, riwaya ya Pepo ya Mabwege (Mwakyembe, 1980) inatia hamasa
Kitabu cha Mwanafunzi 61
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 61 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 61