Page 67 - Fasihi_Kisw_F5
P. 67
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
7. “Hadithi fupi ni utanzu usioeleweka” Jadili kauli hii kwa mifano.
8. Jadili maendeleo ya riwaya ya Kiswahili baada ya Uhuru.
9. Eleza mchango wa mapinduzi ya viwanda katika kuzuka na kukua kwa
FOR ONLINE READING ONLY
riwaya.
10. Kwa kutumia mifano thabiti, jadili kauli kuwa fasihi simulizi ni malighafi
ya fasihi andishi.
Uhusiano baina ya fasihi simulizi na fasihi andishi
Licha ya kutofautiana, aina za fasihi zina uhusiano wa mwingiliano. Kwa mfano,
kazi za fasihi andishi zina vipengele vya kifasihi simulizi kama vile semi, nyimbo
na mazungumzo au dayolojia, wahusika wasio wanadamu (kwa mfano wanyama,
mazimwi, wadudu na vinginevyo) na mbinu za uwasilishaji (mianzo na miisho
ya hadithi, mianzo na miisho ya tenzi na nyinginezo). Mbali na mwingiliano,
aina hizi za fasihi hutofautiana, kama inavyooneshwa katika jedwali lifuatalo:
Tofauti kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi
Na. Kigezo Fasihi simulizi Fasihi andishi
1. Utunzi Huweza kutungwa mapema Hutungwa kwa
na kukaririwa kabla ya kipindi kirefu kabla ya
uwasilishaji. Huweza pia kuwasilishwa kwa hadhira.
kutungwa papo hapo wakati
wa utendaji.
2. Uwasilishaji Huwasilishwa kwa njia ya Huwasilishwa kwa njia ya
mdomo, ishara na vitendo. maandishi.
Uwasilishaji huo hutumia
viambato kama vile maleba,
miondoko na sauti.
3. Umri Ni kongwe kwa sababu Ilianza baada ya
ilianza kabla ya ugunduzi mwanadamu kugundua
wa maandishi. maandishi.
4. Umiliki Tanzu nyingi za fasihi Ni mali ya mtunzi na
simulizi ni mali ya jamii mdhamini wake.
nzima.
56 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 56 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 56