Page 64 - Fasihi_Kisw_F5
P. 64
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
msanii za kumfanya msomaji awatuhumu watu wasiohusika ndizo zinazojenga
maswali akilini mwa msomaji.
(ii) Hutumia wahusika wa kimwendelezo
FOR ONLINE READING ONLY
Riwaya pendwa zina sifa ya kutumia wahusika walewale; hivyo, huwa na
uwezo wa kujiendeleza katika vitabu kadhaa. Karibu kila mwandishi maarufu
wa riwaya pendwa ameandika vitabu zaidi ya kimoja. Sifa hiyo ya kuwatumia
wahusika walewale hufanya kitabu kimoja katika mfuatano wa vitabu kadhaa
vya mwandishi mmoja kionekane kama tukio linalojitegemea katika mfululizo
wa matukio mengi. Mifano ya watunzi waliowatumia wahusika wa jinsi hii
ni Aristablus Elvis Musiba. Huyu amemtumia mhusika Willy Gamba katika
riwaya zake. Pia, Muhammed Said Abdulla amemtumia mhusika Bwana Msa
katika riwaya zake takribani zote. Mwandishi mwingine ni Ben Mtobwa ambaye
amemtumia mhusika Joram Kiango katika baadhi ya riwaya zake.
(iii) Huwa na mhusika mkuu mkwezwa
Mhusika wa riwaya pendwa mara nyingi hupewa sifa zisizo za kawaida kitabia
na kiutendaji. Mhusika mkuu wa riwaya pendwa hukwezwa juu ya wahusika
wengine; hivyo, anatawala na ana sifa ya ubabe. Wahusika hawa huwa na sifa
ya kuwa kielelezo chenye ukamilifu, yaani kutokuwa na dosari. Mifano mizuri
ya wahusika wa namna hii ni Bwana Msa, Willy Gamba na Joram Kiango. Mara
kwa mara, mhusika mkuu ndiye mshindi hata akipitia katika taabu na mashaka
ya aina gani, tunajua, hatimaye ataibuka kuwa mshindi katika mapambano yake.
Wahusika hawa wakuu hutenda na kuendesha mambo yao kama miungu wadogo
pasi na kukosea. Huwa hodari sana katika kutenda mambo yao. Mambo hayo
ni kama vile kuchunguza, kufanya mapenzi, kuwindana, kupigana kwa silaha
na kwa mikono mitupu. Kwa hiyo, ufundi wa utendaji unaojitokeza humo
huwa unaziteka nafsi za wasomaji na, wakati mwingine, kuwasahaulisha hata
maudhui. Mfano mzuri ni mhusika mkuu wa riwaya ya Njama (Musiba, 1981).
Msomaji anapoendelea kuisoma riwaya hii, anajikuta anamezwa na ufundi wa
kupeleleza na kupambana unaooneshwa na Willy na wenzake kiasi cha kupoteza
kiini cha simulizi yenyewe, ambacho kinahusu ukombozi wa nchi za Afrika. Hali
hii inasababishwa na hali ya kukwezwa kwa wahusika wa riwaya, hususani Willy
Gamba, katika tabia na matendo yao.
(iv) Hupendwa na watu wengi
Riwaya hizi zina wasomaji na wapenzi wengi, hasa vijana. Hii ni kwa sababu
wasanii wake wameupatia vizuri utunzi wa kisasa ambao umeletwa na utamaduni
Kitabu cha Mwanafunzi 53
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 53 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 53