Page 65 - Fasihi_Kisw_F5
P. 65
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
wa kigeni unaofuatwa kwa makini na vijana na baadhi ya watu wazima. Kwa
hiyo, watu wanaposoma riwaya hizi, wanasisimka na kuburudika.
(v) Hutumia mandhari ya mijini
FOR ONLINE READING ONLY
Wasanii wa riwaya pendwa hutumia mandhari halisi au ya kubuni, hususan katika
miji au majiji. Hali hii ndiyo inayoonesha upekee wa mandhari ya riwaya pendwa.
Wasanii hutumia mandhari ya namna hii ili kukidhi malengo ya usukaji wa visa
na maisha ya wahusika. Mandhari ya namna hii hubeba matukio kama vile ufujaji
mkubwa wa fedha kwenye sehemu za starehe, kama vile baa, hoteli kubwa na
fukwe za bahari. Kwa mfano, kwenye riwaya ya Salamu Toka Kuzimu (Mtobwa,
1987), kuna ufujaji mkubwa wa fedha unaofanywa na mhusika Joram na mpenzi
wake. Vilevile, mandhari ya mjini yanaoneshwa kupitia tukio kama la uchezaji
wa kamari linalojitokeza kwenye riwaya ya Simu ya Kifo (Katalambula, 1965).
Aidha, mandhari ya mjini au jijini yanathibitishwa na kuwapo kwa kampuni na
mashirika makubwa. Kampuni hizi huajiri watu. Waandishi huumba wahusika
wenye vyeo kwa kuhusianisha na kampuni na mashirika hayo. Mfano mzuri ni
mhusika Kalulu katika riwaya ya Pesa Zako Zinanuka (Mtobwa 1984). Huyu ni
kiongozi katika kampuni mojawapo ya kusambaza dawa za Oxton. Mzee Jacobo
kwenye Simu ya Kifo (Katalambula, 1965) ni mfanyakazi katika shirika la reli.
Mandhari ya mijini pia hudhihirika kupitia matumizi ya vyombo vya mawasiliano
kufanikisha matukio ya ujambazi, ujasusi, uporaji na uhusiano wa kimapenzi.
Mathalani, katika riwaya ya Najisikia Kuua Tena (Mtobwa, 1985), mhusika
Kwame anatega chombo cha kunasa mawasiliano ofisini kwa Kombora. Chombo
hiki kinamsaidia kunasa maongezi yote ya mipango ya kuwasaka wahalifu
(Kwame na kundi lake). Kwa njia hii, Kwame na kundi lake wanang’amua
mikakati ya kukamatwa, hivyo, wanafanikiwa kuwakimbia askari.
(vi) Matumizi ya wanawake kama nyenzo ya mafanikio
Kwa ujumla, wahusika wakuu wa kiume wa riwaya pendwa husawiriwa
wakifanikiwa katika mambo yao kupitia mbinu ya kuwatumia wanawake
warembo. Warembo hao hutumiwa kwa njia za mapenzi, kuwa chambo cha
kufanyia uhalifu, au chambo cha kumnasia adui. Mapenzi, kwa upande wake,
huonekana kuwa jambo muhimu sana katika riwaya pendwa. Huonekana
kwamba, upelelezi au shughuli yoyote inayofanyika haiwezi kusisimua wala
kufanikiwa bila mapenzi. Katika riwaya za Musiba, kwa mfano, mhusika Willy
Gamba huwa na wasichana warembo ambao ndio wapenzi wake wanaomsaidia
kufumbua mafumbo mazito na mitego mikubwa. Baadhi yao ni Zabibu kwenye
54 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 54 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 54