Page 66 - Fasihi_Kisw_F5
P. 66
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
riwaya ya Njama, (Musiba 1986), Tete na Mwadi kwenye riwaya ya Kikosi cha
Kisasi, (Musiba 2018), pamoja na Nyaso kwenye riwaya ya Hofu (Musiba 2018).
(vii) Huiga mawazo na matendo ya filamu za kigeni
FOR ONLINE READING ONLY
Riwaya pendwa nyingi za Kiswahili, hasa za miaka ya 1980, ni mwigo wa
maandishi ya Kimagharibi pamoja na filamu za Kizungu na Kiasia zinazohusu
upelelezi, ujasusi, uhalifu na mapenzi. Wasomaji wengi wameifanya riwaya
pendwa kama kibadala au kijalizo cha filamu. Kwa mfano, Musiba kwenye
riwaya zake amemchora mhusika mkuu, Willy Gamba, kwa kumpa ujuzi wa
kupigana kininja katika mapambano dhidi ya majasusi. Kupigana kwa kufuata
sheria za kininja, mara nyingi, ni mbinu zinazotumiwa na filamu za Kimagharibi
na Kimashariki.
Shughuli 2.15
Soma riwaya na hadithi fupi teule, kisha eleza tofauti ya tanzu hizo.
Zoezi la 2.3
1. Kwa kutumia mifano, tofautisha dhana zifuatazo:
(a) melodrama na ramsa
(b) utao na ukwapi
(c) riwaya za kihistoria na za sira
(d) mashairi na tenzi
(e) riwaya za kifalsafa na za kisaikolojia
2. “Riwaya ni zao la fasihi simulizi.” Jadili
3. “Tamthiliya za Kitanzania za sasa ni zao la tamthiliya za Kimagharibi.”
Jadili.
4. Eleza kwa ufupi namna dhana ya utendaji inavyojitokeza katika
tamthiliya.
5. Kwa kutumia mifano, eleza aina za tamthiliya na namna
zinavyotofautiana.
6. Kwa kutumia mifano, jadili mabadiliko ya ushairi wa Kiswahili katika
vipindi mbalimbali.
Kitabu cha Mwanafunzi 55
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 55 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 55