Page 61 - Fasihi_Kisw_F5
P. 61
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
(f) Riwaya za istiara
Hizi ni riwaya za mafumbo ambazo umbo lake la nje ni ishara au kiwakilishi
tu cha jambo jingine. Mifano mizuri ni riwaya za Kusadikika (Robert, 1991) na
Kufikirika (Robert, 1968) ambazo huenda ni istiara kuhusu utawala wa mabavu
FOR ONLINE READING ONLY
wa kikoloni.
(g) Riwaya za kingano
Hizi ni riwaya zenye umbo na mtindo wa ngano. Mathalani, huweza kuwa na
wahusika wanyama, visa vya ajabuajabu, mandhari ya kubuni na visa vyenye
kutendeka nje ya wakati wa kihistoria. Mfano wa riwaya za kingano ni Adili na
Nduguze (Robert, 1952) na Lila na Fila (Kiimbila, 1966).
(h) Riwaya teti
Hizi ni riwaya zinazosimulia vituko na masaibu ya maayari (watu wapuuzi,
laghai, wajanja, na kadhalika) kwa njia inayosisimua na kuchekesha. Aghalabu
maayari hao huwa watu wanaovutia (si wahusika wawi/waovu), wanatokea
tabaka la chini, na bapa. Matukio ya riwaya hii hayana msuko ulioshikamana
vizuri.
(i) Riwaya barua
Hizi ni riwaya ambazo sehemu yake kubwa husimuliwa kwa njia ya barua
wanazoandikiana baadhi ya wahusika. Mfano ni riwaya ya Barua Ndefu kama
Hii (Mariama Bâ, 2009).
(j) Riwaya za kihistoria
Riwaya hizi huchanganya historia halisi na ubunifu ili kutoa maudhui fulani.
Mara nyingi, riwaya hizi zinajikita kwenye matukio makuu ya kihistoria
yaliyoathiri mwenendo na mwelekeo wa jamii au taifa linalohusika. Riwaya ya
kihistoria huchanganya wahusika wa historia na wa kubuni, matukio ya kweli
na ya kubuni. Hata hivyo, riwaya hizo huzingatia zaidi namna matukio makuu
ya kihistoria yalivyomwathiri mtu binafsi aliyeyashiriki. Riwaya ya kihistoria
ina dhamira zinazogusa watu wengi, ni muhimu kwa sababu masimulizi
yake yanahusu mambo yaliyotokea, na inawezekana yaliwahi kuwapata hata
wasomaji. Ni kumbukumbu nzuri ya kipindi kilichopita. Baadhi ya riwaya
mashuhuri za kihistoria ni Uhuru wa Watumwa (Mbotela, 1934), Kuli (Shafi,
1979), Zawadi ya Ushindi (Mtobwa, 1987), Kwa Heri Iselamagazi (Mapalala,
1992) na Pambazuko Gizani (Mboneko, 2004). Pia, kuna riwaya za Mulokozi za
Ngome ya Mianzi (1990), Ngoma ya Mianzi (1991) na Moto wa Mianzi (1996).
Nyingine ni Miradi Bubu ya Wazalendo (Ruhumbika, 1992) na Wachamungu wa
Bibi Kilihona (Ruhumbika, 2014).
50 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 50 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 50