Page 57 - Fasihi_Kisw_F5
P. 57
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
na Shaibu Faraji, na kuchapishwa na William Hichens (1928). Maandiko haya
yalitokea wakati wa kipindi cha Wajerumani (Njogu na Chimerah, 1999).
Baada tu ya Vita vya Kwanza vya Dunia, Waingereza walijishughulisha zaidi na
kuandika na kufasiri vitabu vya shule vya kiada na ziada. Baadhi ya vitabu hivyo
FOR ONLINE READING ONLY
ni: Hadithi ya Allan Quartermain (Haggard [mf.] Frederick Johnson, 1934),
Safari za Gulliver (Swift, [mf.] Frederick Johnson, 1932), Mashimo ya Mfalme
Sulemani (Haggard, [mf.] Edwin Brenn, 1929), Alfu Lela Ulela ([Waf.] Frederick
Johnson na Edwin Brenn, 1929), na Kisiwa Chenye Hazina (Stevenson [mf.]
Frederick Johnson, 1929). Maandiko haya yalikuwa maarufu hadi kufikia mwaka
wa 1950 ambapo waandishi wazawa walianza kujitokeza kuandika nathari za
kibunifu (bunilizi) kwa mfuatano wa kimikondo (Madumulla, 2009).
Riwaya ya Kiswahili iliendelea kukua na kubadilika sambamba na vipindi
mbalimbali vya kihistoria nchini Tanzania. Katika kipindi cha miaka 1940 mpaka
1970, riwaya za aina mbalimbali ziliandikwa, zikiwamo za kitawasifu, kimaadili,
kiutamaduni, na za kihalifu au kikachero. Kwa mfano riwaya za kimaadili, zina
sifa za kifasihi simulizi ambazo ni matumizi ya dialojia, kutofungwa na wakati
pamoja na matumizi ya balagha (chuku), ambayo hukipatia kitu sura, uwezo
na nguvu isiyokuwa ya kawaida. Mifano ya riwaya hizi ni Kusadikika (Robert,
1991), Kufikirika (Robert, 1968) na Adili na Nduguze (Robert, 1952).
Riwaya za kiutamaduni zilisheheni maudhui yaliyosawiri tamaduni za jamii
mbalimbali. Mfano mmojawapo ni riwaya ya Kurwa na Doto (Farsy, 1960)
inayosawiri maisha ya watu wa visiwa vya Unguja na Pemba. Halikadhalika,
kuna riwaya ya Mzishi wa Baba ana Radhi (Nkwera, 1967), inayoelezea maisha
ya Wapangwa wa mkoa wa Njombe, wilayani Lubewa. Vilevile, kuna riwaya
ya Bwana Myombekere na Bibi Bugonoka, Ntulanalwo na Bulihwali (Kitereza,
1980) ambayo inasawiri mila na desturi za jamii ya Wakerewe kabla ya kuja kwa
wakoloni.
Riwaya za kihalifu au kikachero zilibeba maudhui ya uhalifu na upelelezi.
Mifano mizuri ni riwaya za Muhammed Said Abdulla ambazo ni Mzimu wa Watu
wa Kale (1957), Kisima cha Giningi (1968), Duniani kuna Watu (1973), Siri ya
Sifuri (1974) na Mwana wa Yungi Hulewa (1976).
Baada ya uhuru, na hatimaye Azimio la Arusha kutangazwa, ziliibuka riwaya
zenye maudhui yanayohusu siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. Katika kipindi hiki,
makundi mawili ya waandishi yalijitokeza kuandika riwaya kuelezea Azimio la
Arusha. Kundi la kwanza liliuona ujamaa kwa jicho la ujadi. Kundi hili liliandika
46 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 46 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 46