Page 54 - Fasihi_Kisw_F5
P. 54
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Tofauti baina ya michezo ya fasihi simulizi na tamthiliya za fasihi andishi
Michezo ya fasihi simulizi hutofautiana na tamthiliya za fasihi andishi kwa
vipengele vifuatavyo:
(a) Utunzi wa maonesho
FOR ONLINE READING ONLY
Mara nyingi mtungaji wa mchezo na mwigizaji wa tamthiliya huwa tofauti.
Maneno ya mtunzi ni lazima yakaririwe na waigizaji jinsi yalivyo au kama
madokezo ya lazima. Kwa upande wa fasihi simulizi, mara kadhaa watunzi
wa mchezo ndio wachezaji. Maneno na vitendo ni vyao wenyewe na wakati
mwingine hubuniwa papo kwa papo.
(b) Maandalizi
Tamthiliya hupitia maandalizi kadhaa kama vile kufanya mazoezi mengi kabla ya
kuigizwa jukwaani. Pia, jukwaa na vyombo vitakavyotumika sharti viandaliwe
mapema. Kwa ujumla, igizo lolote ili livutie watazamaji linapaswa kufanyiwa
maandalizi mazuri. Kwa upande wa maandalizi drama zinazotokana na vitabu na
zile zinazotungwa tu kichwani lazima ziandaliwe vizuri.
(c) Shabaha
Shabaha kuu katika drama na maigizo ya kawaida ni kuelimisha, kuburudisha na
wakati mwingine ni biashara kwa sababu watu hununua tamthiliya au huuza kazi
hizo katika vituo vya runinga na redio. Vilevile, maigizo huoneshwa ukumbini
ambapo watazamaji hupaswa kulipia.
Shughuli 2.13
Kwa kutumia vyanzo vya maktabani, soma tamthiliya mbili au zaidi, kisha
bainisha aina ya tamthiliya hizo.
Shughuli 2.14
Kwa kutumia vyanzo mbalimbali, jadili dhana na aina za riwaya.
Riwaya
Riwaya ni hadithi ndefu ya kubuni itumiayo lugha ya kinathari (lugha ya mjazo)
yenye uchangamani wa visa, wahusika, mandhari na dhamira. Mara nyingi
vipengele hivyo huakisi maisha ya jamii inayohusika. Hivyo, riwaya huweza
kutoa picha ya jumla ya maisha ya mtu kutoka nyumbani (mtu binafsi) hadi
kiwango cha taifa na hata dunia nzima (Mohamed, 1995; Madumulla, 2009; na
Senkoro, 2011).
Kitabu cha Mwanafunzi 43
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 43 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 43