Page 52 - Fasihi_Kisw_F5
P. 52
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
1969), Mashetani (Hussein, 1971), Hatia (Muhando, 1972), Tambueni Haki Zetu
(Muhando, 1973), Aliyeonja Pepo (Topan, 1973) na Pambo (Muhando, 1975).
Nyingine ni Sundiata (Mbogo, 1975), Jogoo Kijijini na Ngao ya Jadi (Hussein,
1976), Machozi ya Mwanamke (Ngozi, 1977), Mukwava wa Uhehe (Mulokozi,
FOR ONLINE READING ONLY
1979), Arusi (Hussein, 1980), Tendehogo (Semzaba, 1984), na Giza Limeingia
(Mbogo, 1980). Vilevile, kulikuwa na Njia Panda (Muhanika, 1981) Tone la
Mwisho (Mbogo, 1981), Nguzo Mama (Muhando, 1982), Lina Ubani (Muhando,
1984), Kwenye Ukingo wa Thim (Hussein, 1988), Pungwa (Mohamed 1988),
Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe (Semzaba, 1988) Kivuli Kinaishi (Mohamed
1990), na Morani (Mbogo, 1993).
Tamthiliya zimeendelea kutungwa zikiakisi mabadiliko ya mifumo ya maisha
ya jamii ya wakati huo. Mathalani, tamthiliya kama Ushuhuda wa Mifupa
(Ngozi, 1990) na Kilio Chetu (Medical Aid Foundation, 1995) zimejadili kuhusu
maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI katika jamii.
Miaka ya karibuni, tamthiliya ya kihistoria imeanza kushamiri tena baada ya
kupotea kwa takribani miongo mitatu tangu enzi za Kinjekitile na Mukwava
wa Uhehe. Mtunzi aliyejipambanua zaidi katika mkondo huu ni Emmanuel
Mbogo ambaye ametoa tamthiliya nne katika miaka ya karibuni. Tamthiliya hizi
zinaongeza idadi ya tamthiliya zake nyingine mbili za kihistoria alizozichapisha
hapo kabla. Nazo ni Ngoma ya Ng’wanamalundi (1988), Sundiata (1994), Fumo
Lyongo (2009), Sadaka ya John Okello (2015), Nyerere na Safari ya Kanaani
(2015), Malkia Bibi Titi Mohamed (2016) na Shujaa Mirambo (2021). Tamthiliya
hizo, mbali na kupevua mkondo wa tamthiliya ya kihistoria, zinadhihirisha
namna historia inavyoweza kutumika kisanaa kusawiri migogoro na masuala
yenye umuhimu katika jamii ya leo.
Aina za tamthiliya
Tunaweza kuainisha tamthiliya kwa kutumia vigezo mbalimbali kama vile kigezo
cha maudhui, kusudio, dhima, muktadha wa utendaji, hadhira lengwa na mbinu
za kisanii. Kila kigezo hutupatia aina mahususi za tamthiliya. Mathalani, kigezo
cha hadhira lengwa kinapotumika, huweza kutupatia aina zifuatazo: tamthiliya ya
watoto, tamthiliya ya vijana, tamthiliya ya watu wazima, tamthiliya ya wanawake,
tamthiliya ya wanaume, tamthiliya ya miungu na tamthiliya ya waumini wa dini
fulani. Uainishaji uliotumika katika kitabu hiki umetumia kigezo cha mbinu za
kisanaa. Kwa kuzingatia kigezo hicho, tunapata aina zifuatazo: tanzia, ramsa,
tanzia ramsa, na melodrama.
Kitabu cha Mwanafunzi 41
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 41 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 41