Page 48 - Fasihi_Kisw_F5
P. 48
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
3. Majonzi hayaneneki, kila nikikumbukia,
Nawaza kile na hiki, naona kama ruia,
Mauti sijasadiki, kuwa mwisho wa dunia,
FOR ONLINE READING ONLY
Mapenzi tuliyofunga, hapana wa kufungua.
Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini (Robert, 2003:5)
Maswali
(a) Andika ujumbe wa shairi.
(b) Bainisha mloto wa ubeti wa pili.
(c) Bainisha vina vya kati na vya mwisho vya ubeti wa pili.
(d) Orodhesha utao wa ubeti wa kwanza na ukwapi wa ubeti wa tatu.
(e) Orodhesha mizani ya uketo wa kibwagizo cha shairi hili.
Shughuli ya 2.10
Kwa kutumia vyanzo vya mtandaoni na maktabani, jadili dhana na historia ya
hadithi fupi ya Kiswahili.
Hadithi fupi
Hadithi fupi ni simulizi za kubuni zinazosawiri tukio, tabia, mgogoro au kipengele
cha maisha kwa ufupi. Hadithi za namna hii huwa na tukio moja au mawili na
hutumia mawanda finyu. Kwa kawaida, hadithi fupi haina uchangamano mkubwa
wa matukio, na hutumia wahusika wachache.
Historia ya hadithi fupi
Chimbuko la utanzu wa hadithi fupi ni hadithi simulizi na andishi zinazopatikana
katika lugha nyingi duniani. Baadhi ya fani zilizochangia kuchipuka kwa hadithi
fupi ni ngano, hekaya, visa, michapo na tendi. Kuzuka kwa fani ya hadithi fupi
huko Marekani na Ulaya katika karne ya 19 kulisaidiwa sana na kuchipuka kwa
utamaduni wa kusoma magazeti, kwani visa vingi vilichapishwa katika magazeti
hayo. Uhusiano huu kati ya hadithi fupi na magazeti au majarida bado upo hadi
leo.
Historia ya hadithi fupi haitofautiani sana na historia ya riwaya ya Kiswahili.
Visa vya mwanzo vilivyochapishwa kwa Kiswahili ni mkusanyiko wa hekaya
na ngano. Baadhi ya hadithi hizo ni zile zinazopatikana katika vitabu vifuatavyo:
Kitabu cha Mwanafunzi 37
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 37 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 37